WAZIRI wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Innocent Bashungwa akizungumza katika uzinduzi wa mfumo maalumu wa utambuzi wa wakalimani ili kurahisisha upatikanaji wa ajira zao katika mataifa mbalimbali katika hafla iliyofanyika Baraza la Kiswahili la Taifa(BAKITA) leo Makumbusho jijini Dar es salaam.
WAZIRI wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Innocent Bashungwa akikata utepe wakati akizindua mfumo maalumu wa utambuzi wa wakalimani ili kurahisisha upatikanaji wa ajira zao katika mataifa mbalimbali katika hafla iliyofanyika Baraza la Kiswahili la Taifa(BAKITA) leo Makumbusho jijini Dar es salaam, Katikati ni Naibu Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Mh. Pauline Gekul na Kulia ni Kaimu Mtendaji wa BAKITA Bi.Consolatha Mushi.
WAZIRI wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Innocent Bashungwa, Naibu Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Mh. Pauline Gekul wakisikiliza vifaa maalum vya ukalimani vilivyozinduliwa leo.
Baadhi ya wageni waalikwa na watumishi wa Baraza la Kiswahili Tanzania BAKITA wakiwa katika hafla hiyo.
WAZIRI wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Innocent Bashungwa na Naibu Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Mh. Pauline Gekul wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa vifaa hivyo.
…………………………………………………
WAZIRI wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Innocent Bashungwa mesema wakati huu ambao mataifa mengi hususani yaliyopo ndani ya Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) yanahaha kutafuta wataalamu wengi kwa ajili ya kufundisha na kutafsiri lugha ya kiswahili, BAKITA ina kila sababu ya kuitumia fursa hiyo adhimu na kujenga mfumo wa kuwatambua wataalam waliopo hapa nchini.
Bashungwa ametoa kauli hiyo Dar es Salaam leo wakati akizinduzi vifaa maalumu kwa ajili ya utafsiri wa lugha vilivyonunuliwa na Serikali kwa gharama ya Sh Milioni 187.5 ikiwa ni mpango wake wa kuendelea kukikuza lugha ya kiswahili Duniani.
“Baraza la Kiswahili la Taifa(BAKITA) linatakiwa kwenda na teknolojia kwa kutengeneza mfumo maalumu wa utambuzi wa wakalimani ili kurahisisha upatikanaji wa ajira zao katika mataifa mbalimbali,”. Amesema Bashungwa
Ameongeza na kusema ni muhimu kuwa na utaratibu huo utakaotokana na mfumo huo na kwamba hata kama kuna changamoto ya kuutengeneza mfumo huo Wizara yake ipo tayari kuwasiliana na Wizara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ili kuwasaidia wataalamu ili kufanikisha suala hilo.
Naye Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu wa Bakita Consolatha Mushi mbali akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi ameishukuru Serikali kwa msaada wa vifaa hivyo.
Amesema ununuzi wake utawawezesha watu mbalimbali kujifunza lugha ya ukalimani sambamba na kuongeza idadi ya watafisiri wa lugha nchini.
Alisema vifaa hivyo vilivyofungwa katika chumba maalumu kilichopo makao makuu ya Baraza hilo pia vitatumiwa na wanafunzi wanaosoma katika vyuo mbalimbali vilivyopo nchini.