****************************
19, agost
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
DIWANI wa viti Maalum Kibaha Mjini ,Lidya Mgaya amewaasa wanafunzi wa kike wasithubutu kurubuniwa na kuwa na tamaa ya kupenda vitu vya anasa kama chips na rift za bure ,ili kujiepusha na mimba za utotoni.
Aidha amewasihi kuacha kuhofia masomo ya sayansi na hesabu na badala yake wayapende kama ilivyo masomo mengine.
Akigawa taulo za kike ambazo amepata msaada kutoka kampuni ya KEDs, na kisha kuwapatia wanafunzi wa shule ya sekondari, Mwambisi Forest , Lidya Mgaya alisema ,lengo ni kuongea na wanafunzi wa kike kutojihusisha na mahusiano ya kimapenzi wakati wanasoma.
Aliwasisitiza wasimame kuitafuta elimu kwa bidii na wafauru kusiwe na sifuri wala mimba za utotoni wakiwa wanasoma hivyo wajikite kuzingatia masomo na kuepuka mambo mabaya yatakayowarudisha nyuma kitaaluma.
Diwani huyo alielezea, amejipanga kuanza kampeni ya MWANAFUNZI WA KIKE KATAA MIMBA ZA UTOTONI KATAA ZERO hali itakayosaidia kupunguza changamoto ya kukatisha masomo kwasababu ya mimba, kufeli ama utoro.
Lidya aliishukuru halmashauri ya Mji wa Kibaha, ofisa elimu taaluma na sekondari pamoja na halmashauri na KEDs ambao wamemuunga mkono katika zoezi hilo la kupata taulo za kike.
“Niwasisitize usafi wa mwili na choo kuepuka magonjwa kama U.T.I choo kikiwa kisafi mtajiepusha kupata magonjwa ya aina hiyo ,naweni mikono shuleni na mkiwa majumbani kila wakati ili kujizuia na ugonjwa wa Uviko na mjikinge kwa barakoa.”