Home Mchanganyiko DC NYASA AWATAKA WAFANYABIASHARA KUZITUMIA FURSA ZA KIBIASHARA NYASA

DC NYASA AWATAKA WAFANYABIASHARA KUZITUMIA FURSA ZA KIBIASHARA NYASA

0

*******************************

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Kanali Laban Thomas hivi karibuni, amewataka wafanyabiashara wa Wilaya ya Nyasa kushikamana, kupendana na kuzitumia fursa za kibiashara zilizopo Wilayani Nyasa katika kujipatia maendeleo.

Ameyasema hayo  wakati akiongea na Wafanyabiashara wa Wilaya ya Nyasa katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa katika Kikao chenye lengo la kujitambulisha na kuzitambua kero zinazowakabilki wafanyabiashara Wilayani hapa.

Kanali Thomas amefafanua kuwa, Wilaya ya Nyasa hususani katika Mji wa Mbamba bay ni miongoni mwa miji iliyofunguka na inayokua kwa kasi, hivyo wafanyabiashara wanatakiwa kushikamana ,kupendana, na kuzitumia fursa za kibiashara ili kujiletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kutanua Mji na kuacha kufanya biashara sehemu moja, kimazoea yaani Mbamba bay peke yake na badala yake watanue mji.

Ameongeza kuwa Mji wa Mbamba bay ni pamoja na Kata ya Kilosa na Mtipwili na kwa sasa Makao makuu ya Mji wa Mbamba Bay ni Kilosa, Hivyo wafanyabiashara wanatakiwa kuchangamkia fursa ya kuanzisha biashara mbalimbali mpya katika Kata ya Kilosa na kuacha kubanana katika Mji mkongwe wa Mbamba bay ili watanue Fursa za kibiashara.

“wafanyabiashara kwa mnatakiwa mpendane,mshikamane ili muweze kuzitumia Fursa za kibiashara zinazokuwa kwa kasi katika Mji wa mbamba bay Wilayani Nyasa, acheni tabia ya Ubinafsi ili muweze kupata maendeleo kwa kasi, katika Mji ambao unakuwa kwa kasi mara baada ya kufunguka kwa barabara ya Mbinga hadi Mbamba bay, na kufungua fursa za Biashara mbalimbali.

Wafanyabiashara hao wametaja baadhi ya Changamoto zinazowakabili ni pamoja na bandari ya mbamba bay kutofanya kazi ya kupitisha mizigo, kutoka Mtwara hivyo wafanyabiashara hao wamemuomba mkuu wa Wilaya kutoa msukumo kwa Serikali ili iharakishe,  kuzifanya meli zifanye safari na Mizigo ya kutoka Mtwara kuja Mbamba bay ianze  kuja, ili wafanyabiashara waweze kunufaika na kufanya  biashara.

Kero Nyingine inyowakabili wafanyabiashara hao ni makadirio ya kodi yanayofanyika na Mamlaka ya mapato Tanzania kukadiriwa wakiwa Ofisini badala yake wameomba maafisa wa kodi waende katika eneo la biashara ili waweze kukadiriwa vizuri.

Aidha Mkuu wa Wilaya ametatua kero hizo kwa kuwaagiza maafisa wa kodi kufanya makadirio katika maeneo ya Biashara, na kuwaeleza kuwa suala la Bandari atalifikisha katika Mamlaka husika.

Aidha ametoa wito kwa wafanyabiashara wote kufanya biashara halali na kuhakikisha ulinzi na usalama aidha wanapomtilia mashaka mtu yeyote basi weatoe taarifa mapema katika vyombo vya Ulinzi na Usalama.