KLABU ya Yanga imetambulisha wachezaji wapya wawili, beki wa kulia Djuma Shabani na winga wa upande huo huo, Jesus Mololo wote kutoka AS Vita ya kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Moloko anayekuja kuziba pengo la Mkongo mwingine, Tuisila Kisinda anayehamia RSB Berkane ya Morocco na kwa pamoja wawili hao wanafanya idadi ya wachezaji watano Yanga kutoka DRC.
Wengine ni kiungo Tonombe Mukoko aliyesajiliwa tangu msimu uliopita pamoja na Kisinda na washambuliaji wapya Fiston Mayele kutoka AS Vita pia na Heritier Makambo kutoka Horoya ya Guinea.

Jesus Moloko anakuja Yanga kuziba pengo la Mkongo mwenzake, Tuisila Kisinda
Yanga pia imemsajili makipa wapya wawili, Eric Johola kutoka Aigle Noir ya Burundi na Djigui Diarra kutoka Stade Malien ya kwao, Mali.
Lakini pia Yanga imesajilu wachezaji wapya wazawa watatu hadi sasa, beki wa kushoto, David Bryson kutoka KMC ya Dar es Salaam, winga wa upande huo huo, Dickson Ambundo kutoka Dodoma Jiji FC ya Dodoma na mshambuliaji Yussuf Athumani kutoka Biashara United ya Mara.
Yanga inaendelea na utambulisho wa wachezaji wake wapya kabla ya Jumapili kupanda ndege kwenda Morocco kuweka kambi ya kujiandaa na msimu hadi itakaporejea kwa ajili ya tamasha la Kilele cha Wiki ya Mwananchi Agosti 29.