Home Michezo YANGA SC KUANZA NA RIVERS UNITED YA NIGERIA LIGI YA MABINGWA, SIMBA...

YANGA SC KUANZA NA RIVERS UNITED YA NIGERIA LIGI YA MABINGWA, SIMBA NJIA NYEUPE MAKUNDI ,AZAM NA BIASHARA.

0

VIGOGO wa Tanzania, Yanga SC wataanza na Rivers United ya Nigeria katika Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika Septemba mwaka huu.
Yanga wataanzia nyumbani kati ya Septemba 10 na 12 kabla ya kusafiri kwenda mjini Port Harcourt kwa mechi ya marudiano ya kati ya Septemba 17 na 19.
Wakifanikiwa kuvuka hapo watakutana na mshindi kati ya Fasil Kenema SC ya Ethiopia na Al Hilal ya Sudan.
KMKM ya Zanzibar yenyewe itaanzia nyumbani dhidi ya Al Itihad ya Libya na ikivuka hapo itakutana na Esperance ya Tunisia.
Mabingwa wa Tanzania, Simba SC wao wataanzia Raundi ya pili ya mchujo dhidi ya mshindi kati ya Jwaneng Galaxy ya Botswana na DFC Beme Arrondissement ya Afrika ya Kati.
Katika Kombe la Shirikisho, Azam FC itaanzia nyumbani dhidi ya Horsed FC ya Somalia, Biashara United itaanzia ugenini dhidi ya FC Dikhil ya Djibouti na Mafunzo ya Zanzibar itaanzia nyumbani dhidi ya Inter Clube ya Angola.