Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani akitoa hotuba leo ya uzinduzi wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Igunga
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akitoa maelezo ya utangulizi wakati wa uzinduzi wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Igunga
Mkuu wa Wilaya ya Igunga Sauda Mtondoo akifungua kikao cha uzinduzi wa Baraza la Biashara la Wilaya yake.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Igunga wakiwa katika uzinduzi wa Baraza la oleo
Picha na Tiganya Vincent
************************************
NA TIGANYA VINCENT
MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani ameziagiza Halmashauri za Wilaya kuhakikisha zinasimamia matumizi sahihi ya fedha zinazopewa kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuleta matokeo mazuri kwa jamii.
Ametoa kauli hiyo leo mjini Igunga wakati wa uzinduzi wa Baraza la Biashara la Wilaya.
Balozi Dkt.Batilda amesema ni lazima miradi ya maendeleo inayojengwa katika maeneo mbalimbali ya wananchi ilingane na thamani halisi ya fedha inayotolewa na Serikali.
“Hakikisheni mnasimamia vema utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili ijengwe kwa viwango vilivyokusudiwa na msisite kuchukua hatua kali kwa watendaji ambao watatekeleza miradi chini ya kiwango” amesisitiza.
Ameongeza kuwa sanjari na hilo ni vema Halmashauri zikahakikisha zinaongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato ikiwemo kubuni vyanzo vipya vya mapato ambavyo vitawapatia fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Balozi Dkt. Batilda amesema ukusanyaji wa mapato ni vema ukatumia njia shirikishi na Rafiki kwa wananchi balada ya kusubiri kutoza faini.
“Ukusanyaji wa mapato uwe wa kirafiki zaidi badala ya kugeuza faini kama sehemu ya kukusanya mapato” amesema.