Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) ,Dkt Yusuph Mhando,akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa chuo hicho kwa Waandishi wa Habari waliofika Chuoni hapo katika ziara ya kuangalia maboresho yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika chuo hicho.
Baadhi ya waandishi na wafanyakazi na wanafunzi wakifatilia wasilisho la Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) ,Dkt Yusuph Mhando (hayupo pichaniu) wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa chuo hicho kwa Waandishi wa Habari waliofika Chuoni hapo katika ziara ya kuangalia maboresho yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika chuo hicho.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) ,Dkt Yusuph Mhando,akiwa katika picha ya pamoja na Waandishi wa Habari waliofika Chuoni hapo katika ziara ya kuangalia maboresho yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika chuo hicho mara baada ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa chuo hicho.
Muonekano wa jengo lililopo katika Chuo cha Ufundi Arusha mara baada ya maboresho yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia
Muonekano wa Tenki la Maji lililopo katika Chuo cha Ufundi Arusha mara baada ya maboresho yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia .
Waandishi wa habari wakiendelea kukagua miradi iliyotekelezwa katika Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) wakati wa ziara ya kuangalia maboresho yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika chuo hicho.
Mkufunzi kutoka Idara ya Magari katika Chuo cha Ufundi Arusha,Mhandisi David Raymond akiwaeleza Waandishi wa Habari waliofika Chuoni hapo katika ziara ya kuangalia maboresho yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika chuo hicho jinsi walivyojipanga kuanza kutengeneza gari litakalotumia umeme mara baada ya kupatiwa vifaa vya kisasa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia.
Baadhi ya magari yaliyofanyiwa maboresha katika Chuo cha Ufundi Arusha.
Wanafunzi wakitengeneza mashine ya kutoa sanitaizer ili kujikinga na ugonjwa wa Corona ambayo mtu ataitumia bila kugusa maji ama sabuni mara baada ya kupatiwa vifaa vya kisasa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia.
Muonekano wa mashine zilizopo katika chuo cha Ufundi Arusha
Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo cha Ufundi Arusha ,anaesomea Electrical Biometrical Engineering, Wema Laurence akielezea maboresho yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yatawasaidia kwa kiasi kikubwa katika masomo yao kwani watafika chuo kwa wakati kutokana na kukaa hosteli ambazo zipo karibu na Chuo.
Mkufunzi kutoka Idara ya Magari katika Chuo cha Ufundi Arusha,Mhandisi David Raymond akiendesha baiskeli iliyotengenezwa katika Chuo hicho mara baada ya kupatiwa vifaa vya kisasa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia.
Mwanafunzi wa Mwaka wa tatu Chuo cha Ufundi Arusha Leocadia Shirima akiipongeza Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa kukidhi mahitaji yao kwa upande wa wasichana baada ya maboresho yaliyofanywa katika Chuo cha Ufundi Arusha
Mkufunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha Mhandisi Abdi Mjema akiwaonyesha waandishi wa habari muundo wa kutengeneza ndege mara baada ya kupatiwa vifaa vya kisasi na Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika maboresho yaliyofanywa katika Chuo hicho.
……………………………………………………………………
Na Alex Sonna,Arusha
KUTOKANA na kupatiwa vifaa vya kisasa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kipo mbioni kutengeneza gari litakalotumia umeme.
Hayo yameelezwa leo Agosti 12,2021 na Mkufunzi kutoka Idara ya Magari katika Chuo cha Ufundi Arusha,Mhandisi David Raymond wakati akizungumza na Waandishi wa Habari waliofika Chuoni hapo katika ziara ya kuangalia maboresho yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika chuo hicho.
Mhandisi huyo amesema maboresho yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yamewagusa kwa kiasi kikubwa kwani wameweza kupata vifaa vya kisasa na wanafunzi wanasoma kwa urahisi na wengi wamekuwa wakielewa kutokana na kusoma kwa vitendo.
Amesema kwa sasa wameweza kutengeneza baiskeli pamoja na Helcopta na wapo mbioni kutengeza gari ambalo litatumia umeme kutokana na kupatiwa vifaa vya kisasa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia..
“Tumetengeza baiskeli yenye kutumia umeme wa jua na tuna tunaendelea na utengenezaji wa Helcolta ambao upo katika hatua za mwisho kwa hivi ni vitu ambavyo tumetengeneza kwa sasa lakini tupo mbioni kutengeneza gari kabisa litatumia umeme, vyote vinatengenezwa hapa katika idara yetu”amesema Mhandisi Raymond.
Aidha,Mhandishi huyo amesema chuo hicho kinafundisha ufundi wa umeme wa magari na magari yenyewe ambapo amedai kuna madhara makubwa kupeleka magari kwa mafundi wa mtaani kwani wengi wamekuwa wakifanya kazi kwa kubahatisha.
MABORESHO YA WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Chuo hicho,Kaimu Mkuu wa Chuo hicho ,Dkt Yusuph Mhando amesema chuo hicho kilianzishwa mwaka 1978 kwa madhumuni ya kutoa mafunzo ya ufundi sanifu katika ngazi ya Cheti(Full Technician Certificate – FTC) ili kupata wataalamu wenye sifa na ujuzi katika fani mbalimbali za Ufundi.
Dkt Mhando anasema Chuo cha Ufundi Arusha kilipandishwa hadhi ya kiuendeshaji kupitia Gazeti la Serikali No. 78 la mwaka 2007 na kufanyiwa marekebisho kupitia Gazeti la Serikali Na. 302 la mwaka 2015.
Amesema ATC inatoa mafunzo ya ufundi stadi katika ngazi mbalimbali (level I, II na III) na elimu ya ufundi kwa ngazi za Astashahada, Stashahada na Shahada katika fani mbalimbali katika michepuo ya Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
Kaimu Mkuu huyo amasema chuo hicho kinachoongoza kwa kutoa Mafunzo, Tafiti na Ushauri wa Kitaalamu vinavyoaendana na mahitaji ya soko kwa kutumia Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa Maendeleo Endelevu.
Amesema programu zinazoendeshwa chuoni hapo zimeanzishwa kwa kuzingatia, Sera za Taifa,Soko la ajira,Azimio la Kilimo Kwanza,upungufu wa mafundi wa Maabara za Sayansi katika Shule za Sekondari,Uharibifu wa vifaa tiba hospitalini,Mabadiliko ya teknolojia na utandawazi na teknolojia ya habari na mawasiliano.
Kaimu Mkuu huyo amesema chuo kinatoa Programu za kitaaluma 21 zinazotambuliwa na NACTE na kupewa ithibati.
ZAIDI YA BILIONI 1.4 KWA BWENI LA WASICHANA
Kaimu Mkuu huyo wa amesema Chuo kilipokea jumla ya shilingi 1.499 bilioni – 14/05/2021 kama ruzuku kutoka serikalini kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 420.
“Mradi ulianza mwishoni mwa mwezi Mei, 2021 ambapo utekelezaji umefikia 15% na upo katika hatua za ujenzi wa msingi (substructure),”amesema.
UJENZI WA MEDICAL CLINIC
Kaimu huyo Mkuu wa Chuo amesema ili kuwapatia wanafunzi na watumishi huduma za afya na kwa haraka chuo kilianza ujenzi wa kliniki kwa kutumia mapato yake ya ndani
Amesema Mradi ulianza mwishoni mwa mwezi Aprili, 2021 ambapo utekelezaji umefikia 30% na upo katika hatua za ujenzi wa msingi mkubwa (superstructure-framed structure)
UJENZI WA JENGO LA MADARASA NA MAABARA
Amesema Ujenzi ulianza Machi 2018 na mpaka Disemba 31, 2019 utekelezaji ulifiia 49%. Mkandarasi aliondoka site na Wizara inashughulikia upatikanaji wa fedha za kumalizia jengo kwa force account.
BILIONI 37 MRADI WA NISHATI JADIDIFU
Amesema mradi wa East Africa for Transformation and Regional Integration Project (EASTRIP)’ inalenga uanzishwaji wa Kituo cha Umahiri cha Kikanda katika Nishati Jadidifu.
Amesema thamani ya mradi ni Shilingi 37.4 billion , ambapo Chuo kimeshapokea shilingi 11.2 billion ambayo ni 30% ya fedha yote ya mradi kama kianzio.
BILIONI 7 MRADI WA INNOVATION ENERGY EDUCATION PROGRAM (IEEP)
Amesema IEEP ni mradi unaofadhiliwa na Wizara ya elimu ya Korea ambapo Mradi huo una thamani ya Shilingi bilioni tano kwa kipindi cha miaka saba kuanzia Aprili 2020 mpaka Machi 2027.
Amesema ATC inashirikiana na vyuo viwili vya Korea -Hanyang University na Seoul National University katika kutekeleza mradi huo.
MABORESHO YAWASAIDIA
Kwa upande wake mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo hicho,anaesomea Electrical Biometrical Engineering, Wema Laurence amesema maboresho yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yatawasaidia kwa kiasi kikubwa katika masomo yao kwani watafika chuo kwa wakati kutokana na kukaa hosteli ambazo zipo karibu na Chuo.
“Tunaishukuru Serikali wameanza kutujengea hosteli mpya ambazo zitatuwewezasha sisi kufika darasani kwa wakati, ambao tulikuwa tunakaa nje tunapata changamoto za usafiri tunachelewa kufika sasa hivi tutakuwa tunafika kwa wakati,”amesema.
Kuhusiana na kusoma masomo ya umeme,anasema ndoto zake zilikuwa kuja kuwa Inginia hivyo alivyofika chuoni hapo na msukumo wake ulikuwa katika masomo ya Sayansi alimua kujiunga na kozi ya umeme.
“Mimi nilikuwa napenda umeme na nilivyokuja hapa chuo nikakutana na Biometical nikaelezewa jinsi ilivyo na walionitangulia nikaipenda nikaamua kuingia kwenye Biometical,”amesema
WATENGENEZA MASHINE YA KUTOA SANITAIZER
Amesema wametengeneza mashine ya kutoa sanitaizer ili kujikinga na ugonjwa wa Corona ambayo mtu ataitumia bila kugusa maji ama sabuni.
“Na hii inasaidia kupunguza maambukizi ya Corona kwa sababu Corona inaambukiza kwa kushikana au kwa kusogeleana,Chuo chetu kina wanafunzi na walimu wengi hivyo inatusaidia. Hii mashine imefikia hatua nzuri tunachomalizia ni kufunga ‘sense’ mashine zetu tumezitengeneza kidigital zitakuwa zikitumia solar hivyo zitakuwa zikijichaji huku zikiendelea kutumika,”amesema.