Home Michezo YANGA SC YATAMBULISHA DAVID BRYSON KUTOKA KMC

YANGA SC YATAMBULISHA DAVID BRYSON KUTOKA KMC

0
KLABU ya Yanga imemtambulisha rasmi beki wa kushoto, David Bryson kutoka KMC ya Dar es Salaam kuwa mchezaji wake mpya wa saba kuelekea msimu ujao.
Bryson anakuwa mchezaji mpya mzawa wa tatu baada ya winga
winga, Dickson Ambundo kutoka Dodoma Jiji FC ya Dodoma na mshambuliaji Yussuf Athumani kutoka Biashara United ya Mara.
Wengine wanne ni wa kigeni, makipa Mrundi, Eric Johola kutoka Aigle Noir ya kwao, Bujumbura na Djigui Diarra kutoka Stade Malien ya kwao, Mali na washambuliaji Wakongo Fiston Mayele kutoka AS Vita ya kwao, Kinshasa na Heritier Makambo kutoka Horoya ya Guinea.

Yanga inaendelea na utambulisho wa wachezaji wake wapya kabla ya Jumapili kupanda ndege kwenda Morocco kuweka kambi ya kujiandaa na msimu hadi itakaporejea kwa ajili ya tamasha la Kilele cha Wiki ya Mwananchi Agosti 29.