Webster Kaunga Mkuu wa Kitengo cha Biashara Akiba Commercial Bank akikata utepe wakati benki hiyo ilipozindua huduma za Akiba Wakala katika Tawi la Makao Makuu barabara ya Ohio jana wanaopiga makofi kutoka kulia ni Dora Saria Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Bw. Charles Kamoto Mkuu wa Kitongo cha Mikopo.
Webster Kaunga Mkuu wa Kitengo cha Biashara Akiba Commercial Bank na Bw. Charles Kamoto Mkuu wa Kitongo cha Mikopo wakikata utepe wakati wa uzinduzi huo.
Webster Kaunga Mkuu wa Kitengo cha Biashara Akiba Commercial Bank na Bw. Charles Kamoto Mkuu wa Kitongo cha Mikopo wakifunua kitambaa mara baada ya kukata utepe wakati wa uzinduzi huo.
Dora Saria Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Akiba Commercial Bank amesema benki hiyo imeanzisha huduma ya Wakala ijulikanayo kwa jina la Akiba Wakala.
Huduma hii itawasaidia wateja wa benki hiyo kupata huduma kwa urahisi zaidi popote pale walipo kupitia mtandao mpana wa huduma za Wakala unaopatikana nchi nzima.
Dora Saria ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo kwenye tawi la benki hiyo ililopo baeabaea ya Ohio mkabala nahoteli ya Serena jijini Dar es salaam jana.
Amesema Mteja anaweza kupata huduma ya kutoa na kuweka fedha mahali popote penye tangazo la Akiba Wakala Kupitia huduma hii tutawafikia Watanzania wengi popote pale walipo na wataweza kunufaika na huduma zetu.
Pia ameongeza kuwa kwamba, kupitia huduma hii ya Akiba Wakala Benki watakuwa washiriki wazuri katika kuunga mkono harakati za Serikali za kuhakikisha uwepo wa huduma jumuishi za kifedha yaani (Financial inclusion) kwa Watanzania wote.
Tumeingia sokoni na jumla ya Wakala wapatao 200 na lengo letu ni kuendelea kuongeza Wakala wengi kadri iwezekanavyo kwa lengo la kukidhi kiu ya upatikana wa huduma za Akiba nchi nzima, kwa urahisi na ukaribu kwa kumfata mteja popote alipo au kwa urahisi waweza kusema pasipo na ulazima kwa kufika tawini.
Aidha, Benki itaendelea kuboresha huduma hizi za Akiba Wakala kwa kuhakikisha upatikana wa mahitaji mengi ya kibenki kadri iwezekanavyo kwa Wakala wetu kwa lengo la kuleta urahisi na huduma zaidi kwa wananchi kama tulivyoainisha kwenye kauli mbiu ya huduma hii ya Akiba Wakala ambayo inasema Huduma Zaidi.
“Tunategemea kutoa huduma za kufungua akaunti na nyinginezo nyingi hapo mbeleni. Vile vile Benki imeanzisha mkakati rasmi wa kuhakikisha kuingia rasmi katika mfumo wa kidigitali katika mchakato wa kutoa huduma.”. Amesema Dora Saria
Mfumo huu utaendelea kuleta unafuu na kuokoa gharama za upatikananji wa huduma zetu.Pia tunazo huduma za Akiba Mobile, ambazo zinawawezesha wateja wetu kupata mahitaji mbali mbali ya Kibenki na mengineyo mathalani kununua LUKU, ving’amuzi, muda wa maongezi pamoja na malipo yote ya Serikali kupitia simu zao za mikononi.
Ameongeza kuwa wateja wote wa Benki ya Akiba wanaomiliki akaunti binafsi wanakuwa wameunganishwa na huduma hii na wanaweza kufanya miamala popote pale walipo. Huduma ya Akiba Mobile inaptikana kupitia mfumo wa USSD na App kwa wale wanoatumia simu janja.
Pia huduma ya Akiba Mobile inamuwezesha mteja kufanya miamala yake ya kibenki kupitia Akiba Wakala vile vile.Kabla ya hitimisho naomba pia niwadokeze ndugu wnahabari kuwa Benki ya Akiba inatoa huduma nyingine nyingi za Amana, Mikopo, kuuza na kununua float, kutuma na kupokea fedha kupitia Western Union n.k.
Ametoa rai kwa Watanzania wote watembelee matawi yetu yote pamoja na Akiba Wakala kwa ajili ya kuhudumiwa na ufafanuzi.Kwa kumalizia, ikumbukwe kwamba benki yetu imepata mwekezaji wa kimkakati, ambaye ni National Bank of Malawi (NBM).
Ni imani yetu kwamba ubia huu utasaidia kupanua wigo wetu wa kibiashara ikizingatiwa NBM ni moja ya benki kubwa kwenye ukanda wetu wa nchi kusini mwa Afrika. Vile vile, tutaendelea kuboresha na kuanzisha huduma nyingi zikiwemo za kidijitali na hizi za Akiba Wakala imezinduliwa rasmi na tunawakaribisha Wateja wetu wote watumie huduma hiyo kwa mahitaji yako kibenki na wakumbuke kuwa hawana ulazima wa kufika matawini kwa ajili ya kuweka na kutoa fedha kwenye Akaunti zao, kufanya marejesho ya mikopo