Ndg. Moremi Marwa, Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaa akizungunza na waalikwa waliohudhuria katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye ofisi za DSE Jengo la NHC jijini Dar es Salaam leo Agosti 3,2021.
Irene Madeje Moola Mtendaji Mkuu wa Uendelezaji wa Huduma za Kifedha Tanzania FSDT akizungumza na waalikwa katika hafla hiyo iliyofanyika leo jijini Dar Salaam.
Nicodemus Mkama Afisa Mtendaji Mkuu Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana CMCA akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Nicodemus Mukama Afisa Mtendaji Mkuu Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana CMCA akizindua Mpango wa kuendeleza kampuni za wajasiriamali wadogo na wakati “Mpango wa Endeleza”. katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa na waandishi wa habari waliohudhuria katika hafla hiyo.
…………………………………..
MAMLAKA ya Masoko na Mitaji(CMSA) imewahimiza wawekezaji wa ndani na nje kutumia fursa ya mpango wa kuwekeza katika kampuni ndogo na za kati za ujasiriamali ili ziweze kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi.
Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam na Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo, Nicodemus Mukama kwenye hafla ya uzinduzi wa Mpango wa kuendeleza kampuni za wajasiriamali wadogo na wakati “Mpango wa Endeleza”.
Alisema mpango huu ni matokeo chanya ya ushirikiano wa wadau katika sekta ya masoko ya mitaji,wenye lengo la kuunga mkono juhudi za serikali.
Mukama alisema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana itaendela kujenga mazingira wezeshi na Shirikishi kwa lengo la kufikia azma hiyo kwa maendeleao ya masoko ya mitaji hivyo kuchochea ukuaji a uchumi wetu hapa nchini
Aidha, Mamlaka itaendela kutekeleza mikakati ya kujenga masoko endelevu na yenye ufanisi,ikiwa ni pamoja na namna ambayo masoko ya mitaji yanavyotumika kupata fesha za kutekeleza miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam(DSE) Moremi Marwa alisema kuwa programme hiyo ilikuwa imelenga kuwezesha kampuni ndogondogo na za kati kupata mitaji kabla ya kuorodheshwa kwneye soko la hisa.
Alisema mpango huu unawezesha wajasiriamali wadogo na wakati kukua na kuboresha huduma na hivyo kuchangia pato la Taifa.
Marwa alisiema hatua hii ni muhimu ,kwani ina matokeo chanya katika ukuaji wa sekta binafsi;umma na uchumi wa nchi kwa ujumla.
“Ninayo furaha kubwa kuwajulisha kuwa baada ya mafunzo ,kampuni nane zimekidhi vigezo vinavyoelekezwa na mpango
Alizitaja kampuni hizo kuwa ni Selcom, Raha Beverage Company(RABEC),Victoria Finance ,Finca Microfinance Bank Africa Microfinance Ltd(AML),Techno Image; Reni the Wate Experts; and AKM Gilter Ltd.
Alisema kuwa ukosefu wa mitaji ya muda mrefu ni miongoni mwa changamoto kubwa wajasiria mali wadogo na wakati wanakumbana nayo, hivyo mpango huu utasaidia kupata mitaji kutoka kwa wananchi,”alisema
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha(FSDT) Irene Mlola alieleza kushangazwa na wingi wa makampuni ambayo bado hayajachukua mpaka sasa fursa zilizopo katika soko la hisa la Dar es salaam(DSE).