Mgeni rasmi Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Mwanza Eng. Vedastus Maribe akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo. IMEELEZWA kuwa
kampuni nyingi za wakandarasi wanawake wanaotengeneza barabara kwa kutumia
teknolojia stahiki ya nguvu kazi zitafanikiwa endapo wakandarasi hao watakuwa
na nidhamu ya matumizi ya fedha. Hayo yamesemwa na
kaimu meneja wa tanroads mkoa wa mwanza eng. Vedastus Maribe wakati akifungua
mafunzo wakandarasi wa barabara kwa kutumia teknolojia stahiki jijini Mwanza. Eng. Maribe
amewaasa wakandarasi hao kujielimisha vya kutosha kabla ya kuomba kazi ujenzi
na ukarabati wa miradi ili wapate faida na kukuza kampuni zao. “Jazeni
vizuri tender kwa kuzingatia ukubwa wa kazi, imarisheni usimamizi ili kazi
zikamilike kwa wakati, malengo yatimie na kujikomboa kiuchumi,” amesema
Eng. Maribe. Amehimiza
wakandarasi hao kujisajili ili wapewe miradi mingi na hivyo kukua toka wakandarasi
wadogo hadi wakubwa. Naye mratibu wa
mafunzo hayo Eng. Liberatha Alphonce amewataka wakandarasi hao kuongeza mtandao
wa wadau ili kubadilishana uzoefu, ujuzi na fursa. Amesema Wizara ya
Ujenzi na Uchukuzi ina imani na kazi zinazofanywa na wanawake hivyo itaendelea
kuwajengea uwezo na kuwapa miradi mingi kutokana na bidii zao. Zaidi ya
wakandarasi wanawake 80, toka mikoa ya Mwanza, Simiyu, Mara, Geita na Kagera
wanashiriki mafunzo hayo ambayo pamoja na mambo mengine yatawajengea uwezo
katika ujazaji wa zabuni, taratibu za kusajili kampuni, sheria ya manunuzi,
namna ya kutumia mfumo wa manunuzi (TANePS) na usimamizi wa mikataba. Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano. |