KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa (UVCCM) Kenani Kihongosi akiwaongoza Vijana wa CCM katika matembezi yaliyoanzia katika viwanja vya Nyerere Square hadi Uwanja wa Jamhuri kwenye uzinduzi wa Vijana Jogging Club Dodoma uliofanyika leo Julai 31,2021 jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa (UVCCM) Kenani Kihongosi akishiriki mazoezi kwenye uzinduzi wa Vijana Jogging Club Dodoma uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri leo Julai 31,2021 jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa (UVCCM) Kenani Kihongosi,akizungumza mara baada ya kuongoza matembezi pamoja na kuzindua Vijana Jogging Club Dodoma uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri leo Julai 31,2021 jijini Dodoma.
Mbunge wa Dodoma Mjini (CCM) Anthony Mavunde,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Vijana Jogging Club uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri leo Julai 31,2021 jijini Dodoma.
Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili mbaga,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Vijana Jogging Club uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri leo Julai 31,2021 jijini Dodoma.
Diwani wa Kata ya Sekei Mkoani Arusha,Gerald Sebastian,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Vijana Jogging Club uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri leo Julai 31,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dodoma,Bill Chidabwa,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Vijana Jogging Club uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri leo Julai 31,2021 jijini Dodoma.
…………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa (UVCCM) Kenani Kihongosi amezindua Vijana Jogging Club Dodoma huku akiwaagiza Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa na Wilaya kusimamia uanzishwaji wa Club za Jogging katika maeneo yao.
Akizungumza leo Julai 31,2021 jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Vijana Jogging Club uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Kihongosi amesema kuwa utaratibu huo utasaidia vijana kujikinga na magonjwa ambayo sio ya kuambukiza pamoja na kuiweka miili vizuri.
“Leo tunazindua jogging hii hapa Dodoma lakini tunataka kila mkoa iunde vikundi kama hivi ambavyo vitakuwa vinafanya mazoezi kila mwisho wa mwezi,”amesema Kihongosi
Bw.Kihongosi amefanya mazoezi kuanzia katika viwanja vya Nyerere Square hadi katika uwanja wa Jamhuri pamoja na vijana wa Mikoa ya Arusha,Iringa na Dodoma, wanafunzi wa Vyuo Vikuu,shule za Sekondari na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini,Anthony Mavunde.
“Naagiza Makatibu wa Mikoa ,Wilaya na Wenyeviri Nchi nzima wafanye utaratibu katika Mikoa yao kuanzisha Club kama hizi, niwaombe waende kuyasimamia haya tuende tukasimamie afya ili tukajikinge na hili gonjwa nyemelezi,”amesema
Amesema ufanyaji wa mazoezi unaimarisha kinga za mwili hivyo ni wajibu vijana kujikita kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa ambayo sio ya kuambukiza.
Hata hivyo Kihongosi amewataka vijana kujitokeza kupata chanjo ya ugonjwa wa UVIKO 19 ambayo ni ya hiari huku akisisitiza vijana kuendelea kufanya mazoezi ili kujikinga na ugonjwa huo.
“Chanjo ni hiari tuhamasishe watu wapate chanjo uhai wa mtu ni yeye mwenyewe wale wenye fursa nendeni mkachanje akili za kuambiwa changanya na zako kikubwa fanyeni mazoezi kujikinga na Corona,”amesema Kihongosi
Aidha amewataka vijana kuendelea kulinga amani ya nchi kwa nguvu zao zote na kuepuka mambo ya kichochezi ambayo yatahatarisha aman ya nchi na kusababisha machafuko
”Kulinda amani ya nchi ni wajibu wa kila kijana kwani hakuna mtu ambaye atatoka taifa lingine kuja kulinda amani na inapotoweka makundi yanayoathirika zaidi ni watoto, wazee, na wakina mama”amesisitiza Kihongosi
Kwa upande wake,Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini,Anthony Mavunde amesema anafurahi kuona UVCCM ikihamasisha kuendelea kufanya mazoezi ambapo ameahidi kuendelea kushirikiana na umoja huo kuhakikisha wanafikia malengo.
“Nafurahi UVCCM mnashirikisha vijana ni vyema kuendelea,nikuahidi tutakuwa bega kwa bega kufikia malengo na matarajio,”amesema Mavunde.
Naye,Diwani wa Kata ya Sekei Mkoani Arusha,Gerald Sebastian amesema vijana wa Dodoma wamepata bahati kuwa karibu na Kihongosi kwani ni mchapakazi huku akiwataka kushirikiana nae na wampe ushirikiano ili mambo yaende vizuri.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dodoma,Bill Chidabwa amesema wataendelea kuwa mabalozi wa umoja huo kwa kuhakikisha wanafikia malengo yao waliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi mara kwa mara ili kujikinga na magonjwa ambayo sio ya kuambukiza.