Home Mchanganyiko TAFITI ZA KIAFYA ZIMESAIDIA KATIKA UTUNGAJI SERA NDANI NA NJE YA NCHI-PROF...

TAFITI ZA KIAFYA ZIMESAIDIA KATIKA UTUNGAJI SERA NDANI NA NJE YA NCHI-PROF PEMBE

0

Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof Andrea Pembe akizungumza wakati akifunga kongamano la watfiti wa magonjwa mnalimbali ya binadamu kwenye Chuo Kikuu cha Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) jijini Dar es Salaam.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof Andrea Pembe akikabidhi tuzo kwa Dr.Mark Mayala mshindi wa jumla wa machapisho ya kisayansi.

Picha mbalimbali zikionesha washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia ufungaji wa kongamano.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof Andrea Pembe amesema chuo chake kimekuwa kinafanya kongamano la kisayansi kuhusu tafiti mbalimbali kwa mwaka wa tisa mfululizo.

Prof Pembe amesema kuwa, tafiti hizi zimekuwa zinatumika katika utungaji wa sera za kiafya ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa wakati wa kufungwa na Kongamano la kisayansi lililofanyika kwa siku mbili katika Chuo cha MUHAS lililowakutanishwa wataalam mbalimbali na watafiti, watunga sera na watekelezaji wa huduma za afya.

Prof Pembe amesema, kongamano hilo limekuwa linaangalia masuala mbalimbali hususani magonjwa yasiyoambukiza yaliyopo na yanayoendelea kujitokeza kila siku.

Amesema, katika kongamano hilo watafiti wameangalia changamoto zinazoikumba jamii na namna wanaweza kuwa na fursa kwenye kutafuta ufumbuzi utakaokuwa na tija kwa taifa na hata nje ya nchi.

“Tumeangalia tafiti mbalimbali juu ya ugonjwa wa Uviko 19 na magonjwa mengine yasiyoambukiza ikiwemo Kisukari, Shinikizo la Damu na kansa na namna gani ya kupambana nayo kisayansi.” Amesema Prof Pembe.

“ Kuna habari mbalimbali zimekuwa zinasemwa hazina ukweli wowote na MUHAS tumekuwa tunatoa taarifa mbalimvali kwa jamii ambazo ni sahihi kuhusu Uviko 19,” amesema

Prof Pembe amesema, katika kipindi cha miaka ya 2007 hadi 2012 kuliwahi kutokea milipuko ya homa ya mafua ya mapafu na mediteranea na watafiti walipambana kupata suluhisho la ugonjwa huo.

Amesema, katika chanjo nane ambazo zinatumika kwa sasa za Uviko 19 zote ni salama na zimethibitishwa na Shirika la afya duniani (WHO) na chanjo hizi zimekuwa zinasaidia katika kupunguza makali ya ugonjwa wa Uviko 19 na inamsaidia mgonjwa kutokulazwa au kuwekewa mashine ya kupumua.

Kongamano hilo la kisayansi limeweza kuhudhuriwa na watafiti mbalimbali wa ndani na wa kimataifa na yamekuwa na mchango mkubwa kwa sekta ya afya nchini.