Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, wakati akifungua kongamano la watafiti mbalimbali wa magonjwa ya binadamu linalofanyika Chuo Kikuu cha Sayansi Muhimbili (MUHAS) leo Julai 26,2021 jijini Dar es salaam
Mwenyekiti wa Baraza Muhas, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza katika kongamano la watafiti mbalimbali wa magonjwa ya binadamu linalofanyika Chuo Kikuu cha Sayansi Muhimbili (MUHAS) leo Julai 26,2021 jijini Dar es salaam
Picha zikionesha washiriki mbalimbali wa kongamano hilo la watafiti la watafiti mbalimbali wa magonjwa ya binadamu.
Kongamano hili la tisa la siku mbili la watafiti mbalimbali wa magonjwa ya binadamu, linalofanyika Chuo Kikuu cha Sayansi Muhimbili (MUHAS) litawasaidia watafiti wetu kubadilishana ujunzi na maarifa na kutoa majibu ambayo yataisaida serikali namna ya kupambana na magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza na kuokoa watanzania ambao wengi wao wamekuwa wakiishi na magonjwa hayo sugu.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, wakati akifungua kongamano hilo linalofanyika chuoni hapo leo Julai 26,2021 jijini Dar es salaam
Waziri Profesa Ndalichako ametoa wito kwa watafiti wa magonjwa mbalimbali ya binadamu kutoa matokeo ya tafiti ambayo yatasaidia serikali kuboresha miongozo katika sekta ya afya na kudhibiti maambukizi.
“Mkutano huu unalenga kubadilishana uzoefu na ubunifu kwa wataalamu wetu katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali yanayozikabili jamii zetu”Amesema Profesa Ndalichako.
Amesema kuwa majadiliano yatasaidia watunga sera kuboresha na kukabiliana na changamoto ambazo zinahitaji maarifa ya kisayansi katika kufanyia kazi changamoto hizo.
MUHAS inatarajia kujenga Kituo cha umahiri cha magonjwa ya moyo ili kuendelea kufanya utafititi katika magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo moyo, sukari na shinikizo la damu,” amesisitiza.
Amesema serikali inategemea kupata maoni na mapendekezo ya namna ya kuziwezesha taasisi za afya ili kuhakikisha wanakuwa na watu wenye afya bora kwani haiwezi kufikia uchumi wa viwanda bila kuwa na watu wenye afya bora.
Profesa Ndalichako amezisisitizia tasisi za elimu nchini kuzingatia mwongozo uliotolewa hivi karibuni kuhususiana na namna ya kujikinga na kuzuia na ugonjwa wa COVID 19 ili kuvuka salama katika wimbi la tatu la Corona.
“Nawasisitizia walimu kuhakikisha wanafunzi wanafuata taratibu zote za masuala ya afya shuleni ili kuepuka kuambukizana na kuepuka misongamano isiyokua ya lazima,”. amesema Profesa Ndalichako .
Amemalizia kusema muongozo huo pia unawataka wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa nchini kuzungukia katika shule za msingi na sekondari na elimu ya juu ili kuhakikisha taratibu zote za masuala ya kiafya zinafuatwa na kupunguza msongamano katika vyumba vya madarasa.