Katibu MKuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye ulemavu), Mhe.Tixon Nzunda (kulia) akizungumza na waandishi wa habari Makao makuu ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za Kulevya (DCEA) Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za Kulevya, Kamishna Jenerali Gerald Kusaya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu MKuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye ulemavu), Mhe.Tixon Nzunda (kulia) akizungumza na waandishi wa habari Makao makuu ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za Kulevya (DCEA) Jijini Dar es Salaam .Pembeni yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za Kulevya, Kamishna Jenerali Gerald Kusaya.
***********************************
Kiwango cha uingizaji Madawa ya Kulevya nchini kimepungua kwa asilimia 95 huku kuwa changamoto iliyopo sasa ni kuongezeka kwa matumizi ya madawa ya kulevya aina ya Bangi hapa.
Hayo yamebainishwa na Katibu MKuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye ulemavu), Mhe.Tixon Nzunda,wakati alipokuwa amefanya ziara ya kutembelea Makao makuu ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini (DCEA) Jijini Dar es Salaam na kujionea inavyofanya kazi.
“Kwa sasa matumizi ya madawa ya kulevya aina ya bangi yameongezeka nchini tofauti na miaka ya nyuma huivyo natoa wito kwa Viongozi wa Dini na mashirika mbali mbali kuungana katika kupambana kwenye vita ya matumizi ya Bangi kwani yanaathari kubwa”. Amesema Mhe.Nzunda.
Aidha,Nzunda amewatadhalisha wafanyabiashara wa Madawa ya Kulevya pamoja watumiaji na kudai kuwa Tanzania sio sehemu salama kwao kutokana na mikakati iliyowekwa na Mamlaka hiyo katika kupambana na madawa ya kulevya.
Hata Hivyo,Nzunda amesema serikali ya awamu ya sita itaendelea kutoa nguvu kubwa kwenye Mamlaka hiyo ili kuzidisha vita ya kupambana na madawa ya kulevya nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za Kulevya, Kamishna Jenerali Gerald Kusaya amewaonya wale ambao bado wanajihusisha na biashara na usafirishaji wa madawa ya kulevya kuacha mara moja hivyo mamlaka hiyo itaendelea kuwatafuta kwa kushirikiana na jeshi la polisi pamoja na wananchi.