Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete leo amefika eneo la Shule ya Sekondari ya Kiwangwa kushuhudia uharibifu uliotokana na Moto uliounguza Bweni la Wasichana shuleni hapo. Ammekutana na Katibu Tawala wa Mkoa Pwani Hajat Mwanaasha Tumbo. Wamejadili changamoto hiyo na wamejipanga kudhibiti na kuhakikisha hali inarudi vizuri kimasomo ya wanafunzi waliokumbwa na kadhia hiyo.
Na Mwamvua Mwinyi, Kiwangwa
BWENI la wasichana shule ya sekondari Kiwangwa ,huko Bagamoyo limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia Julai 23 mwaka huu ,na kusababisha hasara ikiwemo magodoro na vitanda kuteketea.
Aidha nguo, sare za shule ,vifaa vya kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne ,kama vitabu ,madaftari vimeteketea kwa moto huo .
Baadhi ya viongozi wa mkoa wa Pwani ,akiwepo katibu tawala Mwanasha Tumbo pamoja na mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ,na diwani wa Kiwangwa Malota Kwaga wamefika kujionea namna bweni hilo lilivyoteketea kwa moto.
Ridhiwani amesema wamefika katika eneo la Shule ya Sekondari ya Kiwangwa kushuhudia uharibifu uliotokana na Moto uliounguza Bweni la Wasichana shuleni hapo.
“Shuleni hapo nimekutana na Katibu Tawala wa Mkoa Pwani Hajat Mwanasha Tumbo, tumejipanga kudhibiti na kuhakikisha hali inarudi vizuri kimasomo.”
.
Ridhiwani alieleza ,chanzo cha moto hakijafahamika hadi sasa lakini wameomba wanafunzi kila mmoja aandike kikaratasi kuandika kipi wanaona kimesababisha.
“Ila msiandike kisichokuwepo kama huna uhakika ni vyema ukaacha kuandika “
Ridhiwani alisema wataungana na wadau kuona namna watakavyosaidia kuwezesha kupatikana kwa magodoro,vitabu na mengine ili kutatua janga lililotokea.
Nae diwani wa Kiwangwa Malota Kwaga alisikitishwa kutokea kwa janga hilo kwani limegusa wanafunzi pia wa kidato cha nne ambao wanatarajia kufanya mitihani.
“Moto huu umetokea saa 1 usiku Julai 22 ,na kuitisha gari la zima moto lakini juhudi haziku zaa matunda kwani moto ulishakuwa mkubwa sehemu kubwa .
Chanzo cha kutokea kwa moto huo bado hakijajulikana hadi sasa.