Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Khamisi Mkanachi, akifungua semina kwa Taasisi ya Maendeleo ya Viziwi Tanzania(TAMAVITA) iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ,kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka,yaliyofanyika leo Julai 20,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Khamisi Mkanachi, akisisitiza jambo kwa washiriki wa semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ,kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka,yaliyofanyika leo Julai 20,2021 jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo kwa Viziwi Tanzania (TAMAVITA) Bw.Kelvin Nyema,akitoa neno la shukrani mara baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Khamisi Mkanachi,kufungua semina kwa Taasisi ya Maendeleo ya Viziwi Tanzania(TAMAVITA) iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ,kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka,yaliyofanyika leo Julai 20,2021 jijini Dodoma.
Washiriki wa mafunzo wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Khamisi Mkanachi,(hayupo pichani) wakati akifungua semina kwa Taasisi ya Maendeleo ya Viziwi Tanzania(TAMAVITA) iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka,yaliyofanyika leo Julai 20,2021 jijini Dodoma.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Bw.Titus Kaguo akiwasilisha mada wakati wa semina kwa Taasisi ya Maendeleo ya Viziwi Tanzania(TAMAVITA) iliyoandaliwa na EWURA iliyofanyika leo Julai 20,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Khamisi Mkanachi,akimsikiliza Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Bw.Titus Kaguo (hayupo pichani) wakati akiwasilisha mada wakati wa semina kwa Taasisi ya Maendeleo ya Viziwi Tanzania(TAMAVITA) iliyoandaliwa na EWURA iliyofanyika leo Julai 20,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Khamisi Mkanachi,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua semina kwa Taasisi ya Maendeleo ya Viziwi Tanzania(TAMAVITA) iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka,iliyofanyika leo Julai 20,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………………………………
Na Alex Sonna,Dodoma
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetoa mafunzo kwa watu wasiosikia (Viziwi) huku Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Khamisi Mkanachi akiitaka kuendelea kujenga uelewa kwa watumiaji wa huduma mbalimbali ili wafahamu haki na wajibu wao.
Akizungumza leo Julai 20,2021 jijini Dodoma wakati akifungua semina kwa Taasisi ya Maendeleo ya Viziwi Tanzania(TAMAVITA) iliyoandaliwa na EWURA, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka,amesema kuwa mojawapo ya majukumu ya EWURA ni pamoja na kujenga uelewa kwa watumia huduma ili wafahamu haki na wajibu wao.
“Ninafahamu kuwa ninyi ni sehemu muhimu yawatumia huduma za EWURA,inawezekana kuna mafundi umeme humu ndani ambao inabidi wawe na leseni ya EWURA vilevile inawezekana kuna wamiliki wa vituo vya mafuta ambao inabidi wawe na leseni za EWURA au tunaweza kuwa na wamiliki wa kampuni za kuzalisha na kusambaza umeme na sote tunatumia maji na umeme huduma ambazo zinadhibitiwa na EWURA,”amesema .
Amesema kuwa matarajio ya semina hiyo itawasaidia kutumiza azma ya Serikali kuwasaidia watanzania kutambua haki na wajibu wao kwa jamii na kwa Serikali yao.
“Na kwa kuwa hapa tuna mafundi umeme 30 basi tunategemea huduma bora zaidi kutoka kwenu na kuongezeka kwa ajira binafsi,” amesema.
Amesema kwa niaba ya Serikali wanatoa shukrani za dhati kwa Menejimenti ya EWURA kwa kukubali ombi la kutoa mafunzo hayo kwani kwa kufanya hivyo wananchi wenye ulemavu wa kusikia watakuwa wanaelewa shughuli za EWURA na mafundi umeme wataweza kutimiza matakwa ya kisheria na kikanuni katika shughuli zao
Kwa upande wake,Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo kwa Viziwi Tanzania (TAMAVITA) Bw.Kelvin Nyema,amesema kuwa chama chao kimefikia hatua ya kuomba kupatiwa mafunzo hayo ili wajengewe uwezo mafundi umeme na mafundi wa nyumba ambao ni viziwi.
“Miongoni mwa viziwi wapo mafundi wa umeme, mafundi ujenzi wa nyumba na tunajua tunahitaji leseni lakini hatujui nini cha kufanyeje, pia viziwi ni watumiaji wa maji na nishati na ndio maana tunahitaji mafunzo,”amesema
Pia amesema kuwa katika mafunzo hayo wameshirikisha washiriki 10 katika kila mkoa kutoka mikoa sita ya Singida, Manyara, Dar es Salaam, Morogoro, Iringa na Pwani.
Awali akiwasilisha mada,Meneja Mawasiliano na Uhusiano EWURA,Titus Kaguo ameeleza kuwa Mafunzo hayo yametolewa kutokana na uongozi wa TAMAVITA kuomba kupewa elimu na uelewa wa masuala ya udhibiti wa nishati na maji hali itakayolenga zaidi kuchochea maendeleo.
Pia Kaguo amezishauri Taasisi nyingine kuona umuhimu wa kutoa mafunzo kwa makundi maalumu ili kuleta hamasa kwa jamii kuwasaidiakatikakutekeleza majukumu ya uzalishaji na kujiiunua kiuchumi.
“Nazishauri Taasisi nyingine kutowaacha wenzetu hawa ambao wanaonekana kama ni watu wa pembeni waliosahaulika kwani nao wana uwezo wa kutumika kujenga uchumi wan chi yetu,”amesisistiza Bw.Kaguo
Ameongeza kuwa hatua hiyo ya mafunzo imekuja kwa kuzingatia kuwa kundi hilo ni wadau muhimu kwa Taasisi hiyo ambapo kati ya Wananchama hao 60 ,3o kati yao ni wadau wa moja kwa moja kwani wana leseni za EWURA.
“Tumetimiza wajibu wajibu wetu kuwajenga na kuwaelimisha ili wawe mabalozi kwa wenzao,jamii imekuwa na tabia za kuwasahau wenzetu wa makundi maalum kwa kufanya hivi itasaidia makundimaalumu kuheshimika na kushirikishwa katika uchumi wa viwanda,”amesema