Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki toka Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Andrew Shirima (kulia) akimkaribisha Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (kushoto) wakati Naibu Waziri alipotembelea Taasisi hiyo kwa lengo la kuona shughuli mbalimbali zinazo fanywa na Taasisi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bi.Leah Kihimbi.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki toka Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Andrew Shirima (kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (kulia) wakati Naibu Waziri alipotembelea Taasisi hiyo kwa lengo la kuona shughuli mbalimbali zinazo fanywa na Taasisi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Meneja wa Usajili toka Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Philemon Kilaka (kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (kulia) wakati Naibu Waziri alipotembelea Taasisi hiyo kwa lengo la kuona shughuli mbalimbali zinazo fanywa na Taasisi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Sanaa toka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi.Leah Kihimbi (kulia) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (hayupo pichani) wakati Naibu Waziri alipotembelea Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kwa lengo la kuona shughuli mbalimbali zinazo fanywa na Taasisi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kusoto ni Afisa Utamaduni Mkuu toka wizara hiyo Bw. Habib Msami.
Meneja Usimamizi wa Fedha na Utawala toka Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA),Baraka Katemba (kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (kulia) wakati Naibu Waziri alipotembelea Taasisi hiyo kwa lengo la kuona shughuli mbalimbali zinazo fanywa na Taasisi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA),James Sagenge (kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (kulia) wakati Naibu Waziri alipotembelea Taasisi hiyo kwa lengo la kuona shughuli mbalimbali zinazo fanywa na Taasisi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (kulia) akisisitiza jambo kwa Menejimenti ya Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) wakati Naibu Waziri alipotembelea Taasisi hiyo kwa lengo la kuona shughuli mbalimbali zinazo fanywa na Taasisi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) mara baada ya Naibu Waziri kutembelea Taasisi hiyo kwa lengo la kuona shughuli mbalimbali zinazo fanywa na Taasisi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Picha na WHUSM – Dar es Salaam
………………………………………………………………
Anitha Jonas – COSOTA, Dar es Salaam.
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul aisisitiza Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kuwatumia Maafisa Utamaduni wa ngazi za Mikoa, Wilaya na Halmashauri kutoa elimu ya masuala ya hakimiliki kwa wasanii na makundi mbalimbali.
Mheshimiwa Gekul ametoa msisitizo huo leo Julai 19,2021 Jijini Dar es Salaam alipotembelea COSOTA kwa mara ya kwanza kufahamu majukumu yao na mikakati yao katika kurahishisha utoaji wa huduma na ukusanyaji wa mirabaha ambapo aliwasihi kuongeza kasi katika kutoa elimu ili waweze kukusanya vizuri.
‘’Jitahidini kuongeza kasi katika kutoa elimu kwa wadau kwa kuwatumia Maafisa Utamaduni kutoa elimu kwa wasanii na kwa nyie Maafisa wa COSOTA na gawaneni mikoa kila mmoja awe na jukumu la kuwasiliana na afisa utamaduni wa mkoa fulani kwa lengo la kusaidia kutoa elimu na kwa mambo ambayo hayajakamilika kama marekebisho ya kanuni harakisheni kukamilisha,’’alisema Gekul.
Pamoja na hayo Naibu Waziri huyo aliipongeza COSOTA kwa namna inavyofanya kazi huku akiwasihi mara baada ya kukamilisha marekebisho ya kwa kanuni wanazofanya kuhakikisha wanawapitisha na kuwaelimisha Maafisa Utamaduni kwa lengo kuweza kuwasaidia ili muweze kukusanya kwa kasi.
Kwa upande wa Kaimu Afisa Mtendaji na Msimamizi wa Hakimiliki Tanzania Andrew Shirima alieleza majukumu mbalimbali ya COSOTA pamoja na kufafanua kuhusu mchakato wa upatikanaji wa mfumo wa wa ukusanyaji wa mirabaha na namna mfumo huo utakavyo kuwa unafanya kazi na kurahisisha ukusanyaji wa mapato.
‘Mwezi huu wa Julai tumesaini mkataba na TTCL kwa ajili ya mfumo waliyouandaa wa kuuza kazi mbalimbali za Sanaa ikiwemo filamu ambapo utakuwa unauza filamu kwa viwango vya kimataifa kama ilivyo Netflix na jukumu la COSOTA katika mfumo huu ni kulinda hakimiliki kwa kazi zote zitakazowekwa katika mfumo huo,’’alisema Shirima.
Halikadhalika Kaimu Afisa Mtendaji na Msimamizi wa Hakimiliki huyo alieleza kuwa hivi sasa COSOTA ipo katika maandalizi ya kuandaa kikao cha kuwatembelea Maafisa Utamaduni katika kila mkoa na kuwapa elimu ili waweze kuifahamu COSOTA na kuweza kushirikiana vizuri katika kuwafikia wadau na kutoa elimu katika ngazi ya mikoa.
******************** *** MWISHO*******************