Waziri wa Tehama na Ubunifu wa nchi ya Rwamda, Bi. Paula Ingabire akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuzungumzia ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania kutembelea na kufanya majadiliano na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Kituo cha taifa cha kuhifadhi Data (Data Center) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). |
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya
Habari, Dk. Faustine Ndugulile amesema nchi za Tanzania na Rwanda zitaendelea
kushirikiana na kujengeana uwezo kwenye sekta ya Tehama ili kuhakikisha zinawasaidia
wananchi wa pande zote kunufaika kupitia eneo hilo.
Waziri Dk.
Ndugulile ameyasema hayo, alipozungumza na vyombo vya habari jijini Dar es
Salaam akiwa na Waziri wa Tehama na Ubunifu wa nchi ya Rwamda, Bi. Paula
Ingabire ambaye amefanya ziara ya siku mbili nchini Tanzania.
Dk.
Ndugulile amesema ziara ya Bi. Ingabire inajumuisha kufanya majadiliano na kubadilishana
uzoefu katika sekta ya mawasiliano kwa pande zote mbili. Aliongeza kuwa Tanzania
na Rwanda ni nchi ambazo zimekuwa na ushirikiano kwa muda mrefu kupitia Shirika
la Mawasiliano la Tanzania na lile la Rwanda na mahusiano ya kibiashara.
“TTCL ni
moja ya wadau anayepeleka mawasiliano katika nchi ya Rwanda na amekuwa akitoa
mawasiliano hayo kwa zaidi ya miaka 10 sasa, hivyo nimemkaribisha Waziri kwanza
aje kuona sehemu ambayo mawasiliano yake ya nchi ya Rwanda yanapita na pili
kuja kubadilishana uzoefu kwa pande zote mbili.
“..Nchini kwetu hii ni Wizara Mpya (Tehama) na
kwa Rwanda kuna hatua ambazo wamepiga katika maendeleo ya Tehama, lakini pia
kuja kuangalia fursa zinazopatikana Tanzania na sisi kuangalia fursa hizo kwa
nchi ya Rwanda,” alisema Waziri Dk. Ndugulile.
Alisema
katika ziara hiyo Waziri wa Rwanda na Tanzania watafanya majadiliano kuangalia
maeneo ambayo wanaweza kubadilishana uzoefu kwa lengo la kuboresha zaidi
mahusiano ya pande zote. Sisi kama Wizara ya Teknolojia na Mawasiliano
tumefarijika sana kwa ujio wa Mh. Waziri wa Tehama na Ubunifu wa nchi ya
Rwamda, Bi. Ingabire ili sasa kuangalia yale ambayo tumekuwa tukiwasiliana kwa
maandishi tuweze kuonana ana kwa ana na hata kujionea uwezo tulionao.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri
Kindamba akizungumza katika ziara hiyo, alisema ziara ya kiongozi huyo licha ya
kudumisha mahusiano baina ya nchi hizo inaendelea pia kukuza mahusiano ya kibiashara
kwani TTCL inatoa huduma za internet nchini Rwanda.
Alisema
katika ukanda wa Afrika Mashariki nchi ya Rwanda ni miongoni mwa mataifa
yaliopiga hatua kubwa kwenye teknolojia (ICT), hivyo ujio wa ziara hiyo ni
fursa tosha kwa Tanzania. Alisema katika majadiliano wamekubaliana kuendelea
kufanya biashara na nchi hiyo pamoja na maboresho zaidi ya kiushirikiano.
Aidha
alibainisha kuwa wamekubaliana kuendelea kubadilishana teknolojia, mafunzo ya
kujengeana uwezo, na TTCL inahakikisha inatumia fursa hiyo vizuri ili kuifanya Tanzania
kuwa kitovu cha mawasiliano katika ukanda wa Afrika Mashariki na Ukanda wa nchi
za SADC kutimiza malengo ya Serikali.
Naye Waziri
wa Tehama na Ubunifu wa nchi ya Rwamda, Bi. Paula Ingabire akizungumza alisema Rwanda
na Tanzania zimekuwa na mahusiano ya kubadilishana teknolojia za kidijitali kwa
muda mrefu takribani zaidi ya miaka 10 hivyo ziara hiyo imekuja kuangalia namna
ya kuboresha zaidi mahusiano hayo.
Alisema
Rwanda licha ya kuwa na mahusiano kibiashara kupitia TTCL imekuwa na utaratibu
wa mashirikiano kati ya taasisi za serikali zinazosimamia mawasiliano yaani
TCRA kwa Tanzania na RURA kwa Rwanda
hivyo ziara yake itaboresha zaidi mahusiano na ushirikiano
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuzungumzia ziara ya Waziri wa Tehama na Ubunifu wa nchi ya Rwamda, Bi. Paula Ingabire aliyoifanya kwa siku mbili nchini Tanzania kutembelea na kufanya majadiliano na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Kituo cha taifa cha kuhifadhi Data (Data Center) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Waziri wa Tehama na Ubunifu wa nchi ya Rwamda, Bi. Paula Ingabire akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuzungumzia ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania kutembelea na kufanya majadiliano na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Kituo cha taifa cha kuhifadhi Data (Data Center) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Kutoka kulia ni Ofisa Mkuu kitengo cha Ubunifu nchini Rwanda, Antoine Sebera, Ofisa Mtendaji Mkuu, ‘Broadband Systems Corporation’ Rwanda, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba wakifuatilia mkutano na wanahabari.
Waziri wa Tehama na Ubunifu wa nchi ya Rwamda, Bi. Paula Ingabire (kulia) pamoja na ujumbe wake akiagana na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile (katikati) mara baada ya mkutano na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Waziri wa Tehama na Ubunifu wa nchi ya Rwamda, Bi. Paula Ingabire akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuzungumzia ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania kutembelea na kufanya majadiliano na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Kituo cha taifa cha kuhifadhi Data (Data Center) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba akizungumza na wanahabari mara baada ya kikao cha majadiliano na Waziri wa Tehama na Ubunifu wa nchi ya Rwamda, Bi. Paula Ingabire pamoja na ujumbe alioambatana nao ambao ni viongozi wakuu wa taasisi zinazo ratibu na kusimamia mawasiliano nchini Rwanda.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Bakari (kushoto) akizungumza kwenye kikao cha pamoja na Waziri wa Tehama na Ubunifu wa nchi ya Rwamda, Bi. Paula Ingabire (wa kwanza kulia) pamoja na ujumbe alioambatana nao (hawapo pichani) katika ziara yake nchini Tanzania.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya
Habari, Dk. Faustine Ndugulile amesema nchi za Tanzania na Rwanda zitaendelea
kushirikiana na kujengeana uwezo kwenye sekta ya Tehama ili kuhakikisha zinawasaidia
wananchi wa pande zote kunufaika kupitia eneo hilo.
Waziri Dk.
Ndugulile ameyasema hayo, alipozungumza na vyombo vya habari jijini Dar es
Salaam akiwa na Waziri wa Tehama na Ubunifu wa nchi ya Rwamda, Bi. Paula
Ingabire ambaye amefanya ziara ya siku mbili nchini Tanzania.
Dk.
Ndugulile amesema ziara ya Bi. Ingabire inajumuisha kufanya majadiliano na kubadilishana
uzoefu katika sekta ya mawasiliano kwa pande zote mbili. Aliongeza kuwa Tanzania
na Rwanda ni nchi ambazo zimekuwa na ushirikiano kwa muda mrefu kupitia Shirika
la Mawasiliano la Tanzania na lile la Rwanda na mahusiano ya kibiashara.
“TTCL ni
moja ya wadau anayepeleka mawasiliano katika nchi ya Rwanda na amekuwa akitoa
mawasiliano hayo kwa zaidi ya miaka 10 sasa, hivyo nimemkaribisha Waziri kwanza
aje kuona sehemu ambayo mawasiliano yake ya nchi ya Rwanda yanapita na pili
kuja kubadilishana uzoefu kwa pande zote mbili.
“..Nchini kwetu hii ni Wizara Mpya (Tehama) na
kwa Rwanda kuna hatua ambazo wamepiga katika maendeleo ya Tehama, lakini pia
kuja kuangalia fursa zinazopatikana Tanzania na sisi kuangalia fursa hizo kwa
nchi ya Rwanda,” alisema Waziri Dk. Ndugulile.
Alisema
katika ziara hiyo Waziri wa Rwanda na Tanzania watafanya majadiliano kuangalia
maeneo ambayo wanaweza kubadilishana uzoefu kwa lengo la kuboresha zaidi
mahusiano ya pande zote. Sisi kama Wizara ya Teknolojia na Mawasiliano
tumefarijika sana kwa ujio wa Mh. Waziri wa Tehama na Ubunifu wa nchi ya
Rwamda, Bi. Ingabire ili sasa kuangalia yale ambayo tumekuwa tukiwasiliana kwa
maandishi tuweze kuonana ana kwa ana na hata kujionea uwezo tulionao.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri
Kindamba akizungumza katika ziara hiyo, alisema ziara ya kiongozi huyo licha ya
kudumisha mahusiano baina ya nchi hizo inaendelea pia kukuza mahusiano ya kibiashara
kwani TTCL inatoa huduma za internet nchini Rwanda.
Alisema
katika ukanda wa Afrika Mashariki nchi ya Rwanda ni miongoni mwa mataifa
yaliopiga hatua kubwa kwenye teknolojia (ICT), hivyo ujio wa ziara hiyo ni
fursa tosha kwa Tanzania. Alisema katika majadiliano wamekubaliana kuendelea
kufanya biashara na nchi hiyo pamoja na maboresho zaidi ya kiushirikiano.
Aidha
alibainisha kuwa wamekubaliana kuendelea kubadilishana teknolojia, mafunzo ya
kujengeana uwezo, na TTCL inahakikisha inatumia fursa hiyo vizuri ili kuifanya Tanzania
kuwa kitovu cha mawasiliano katika ukanda wa Afrika Mashariki na Ukanda wa nchi
za SADC kutimiza malengo ya Serikali.
Naye Waziri
wa Tehama na Ubunifu wa nchi ya Rwamda, Bi. Paula Ingabire akizungumza alisema Rwanda
na Tanzania zimekuwa na mahusiano ya kubadilishana teknolojia za kidijitali kwa
muda mrefu takribani zaidi ya miaka 10 hivyo ziara hiyo imekuja kuangalia namna
ya kuboresha zaidi mahusiano hayo.
Alisema
Rwanda licha ya kuwa na mahusiano kibiashara kupitia TTCL imekuwa na utaratibu
wa mashirikiano kati ya taasisi za serikali zinazosimamia mawasiliano yaani
TCRA kwa Tanzania na RURA kwa Rwanda
hivyo ziara yake itaboresha zaidi mahusiano na ushirikiano huo.
Waziri Bi. Paula
Ingabire katika ziara hiyo aliongozana na viongozi wakuu wa taasisi zinazo
ratibu na kusimamia mawasiliano nchini Rwanda na kutembelea na kufanya
majadiliano ya kimkakati na taasisi za TTCL, Kituo cha taifa cha kuhifadhi Data
(Data Center) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
huo.