******************************
Klabu ya Azam imeshindwa kutamba katika dimba lao la Chamazi mara baada ya kulzamishwa sare ya 1-1 dhidi ya klabu ya Simba Sc katika mchezo wa raundi 33 ligi kuu bara.
Azam FC walianza kupachika bao la kuingoza mnamo dakika ya 43 kupitia kwa kiungo mshambuliaji wao Idd Seleman, ‘Nado’. akipokea pasi murua kutoka kwa kiungo Mudathir Yahaya.
Kipindi cha pili Meddie Kagere dk 84 aliweka mzani sawa na kufanya ngoma iwe ngumu kwa timu zote mbili ambapo Azam FC inagawana pointi mojamoja mbele ya Simba.
Kipindi cha pili Azam FC walipata nafasi mbili za dhahabu mwisho wa siku wakakwama kupata ushindi ambapo Ayoub Lyanga alitaka kupachika bao lakini jitihada za mabeki na kipa hakufanikiwa kutikisa nyavu za wapinzani.