Rai hiyo imetolewa Jana na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Dorothy Gwajima wakati akizindua Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala uliofanyika Kwenye ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.
Dkt.Gwajima alisema Serikali bado inasisitiza matumizi ya tiba Asili hivyo ipo haja ya Taasisi za tafiti na vyuo vikuu kuwekeza kwenye tafiti na dawa watakazozalisha zikidhi mahitaji ya wananchi huku usalama,ubora na ufanisi wa dawa hizo ukiwa umejulikana kutokana na tafiti hizo.
Waziri huyo pia alitoa Rai kwa waganga ambao wamesajili dawa zao kupitia Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala waanze kuuza dawa hizo nje ya nchi kwa kuwa Wizara imeshakamilisha kuandaa muongozo wa kusafirisha dawa za tiba Asili kundi la pili nje ya nchi.
“Nitoe Rai kwa waganga ambao wamesajili dawa kupitia Baraza hili muanze kuuza dawa nje ya nchi,kutumia fursa hiyo kutaongeza thamani ya dawa zetu pamoja na uchumi wa nchi,”.Alisisitiza
Hata hivyo alisema ipo haja ya kuanza kuweka JUHUDI za makusudi Katika kuhakikisha malighafi za dawa hizo zinatunzwa kwa kuanzisha mashamba ya kulima miti dawa kwa lengo la kukidhi mahitaji.
“Hapa nchini asilimia zaidi ya 60 ya wananchi wanatumia tiba asili kabla ya kufika katika vituo vya tiba za kisasa,pia Kuna uwiano wa wananchi 800 kwa Mganga mmoja yaani wananchi milioni 60 waganga 75,000”
Aliongeza kusema Kuna takribani mimea dawa 12,000 hii Ina maana kwamba huduma za tiba Asili Zina wateja wengi Sana vijijini na mijini.
“Usalama wa dawa na matumizi ya dawa za tiba Asili ni Jambo ambalo tunatakiwa kuweka nguvu na mkazo zaidi ili kulinda Jamii yetu Katika hili”.
Aidha,Dkt.Gwajima aliwataka waganga wa tiba asili kuhakikisha kusajili dawa zao kwa utaratibu ambao upo kupitia Baraza la tiba Asili na wahakikishe matangazo ya dawa zao yanafanyiwa upekuzi na Baraza Hilo kabla hayajarushwa Katika vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii”Alisema.
Pia Dkt Gwajima alielekeza kufanyiwa marekebisho ya Sheria au kanuni kwa Kushirikiana na Taasisi ya utafiti na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba(TMDA) ili kuondoa muingiliano wa tafsiri ya masuala ya tiba Asili kwa TMDA kwani majukumu ya Baraza Katika Sheria iliyopo ni kukuza,kuboresha na kudhibiti.
Awali akimkaribisha Waziri wa Afya,Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Abel Makubi alisema Wizara yake ipo tayari kuwasapoti Wajumbe hao Kwenye eneo la Tiba Asili hivyo aliwataka waendelee na spidi Katika kuendeleza tiba asili nchini kwani anatambua zipo dawa zinazotibu na kusaidia wananchi.
Prof.Makubi alisema Wizara imeshatenga fedha kwa ajili ya utafiti na Kujenga eneo lililotengwa na Kama mtendaji yupo tayari kuwapa ushirikiano.
Naye Mwenyekiti wa Baraza hiyo Prof.Hamis Malebo alisema Tanzania ni nchi iliyobarikiwa uoto mbalimbali na hivyo mimea iliyopo inasaidia Bali iliyokosekana ni muingiliano wa tiba asili na Tiba ya kisasa.