Home Michezo KMC FC KUSHUKA DIMBA LA UHURU KUWAKABILI JKT TANZANIA KESHO

KMC FC KUSHUKA DIMBA LA UHURU KUWAKABILI JKT TANZANIA KESHO

0

Kikosi cha KMC FC kesho kitashuka katika Dimba la Uhuru Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo mwingine wa Ligi Kuu soka Tanzania bara dhidi ya JKT Tanzania utakaochezwa saa 14:00 mchana.

Hadi sasa maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa na kwamba kikosi hicho cha wana Kino Boys kimejipanga kuhakikisha kwamba kama Timu inakwenda kupata matokeo mazuri kwa maana ya kuondoka na alama tatu.

KMC FC ambayo inanolewa na Makocha, Kocha Mkuu John Simkoko pamoja na Habibu Kondo imejiandaa vilivyo kuwakabili JKT Tanzania licha ya kuwepo kwa ushindani mkubwa lakini imani na mategemeo ya KMC FC kuhakikisha kuwa ushindi unapatikana kwa hali na mali.

“Tunakwenda kuingia kwenye mchezo mwingine ambao nimgumu kiuhalisia lakini sisi tumejipanga kupambania alama tatu muhimu ambazo kimsingi zipo ndani ya uwezo wetu, kila mmoja anapambania Timu yake kubaki kwenye nafasi nzuri kadhalika pia na KMC FC tunafanya hivyo.

Awali katika duru ya kwanza KMC FC ikiwa ugenini dhidi ya JKT Tanzania ilipoteza mchezo kwa kufungwa magoli mawili kwa bila mchezo ambao ulipigwa katika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma.

Imetolewa leo Julai 14

Na Christina Mwagala

Afisa Habari na Mahusiano wa KMC FC