Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania Profesa Charles Kihampa akizungumza na Waandishi wa Habari (hawamo Pichani) wakati wa Mkutano wake na Waandishi hao akitangaza kufunguliwa rasmi kwa Dirisha la udahili kwa waombaji wa Shahada ya kwanza katika Taasisi za elimu ya Juu kwa Mwaka wa masomo 2021/2022.
Mwanasheria wa TCU Roseline Ruta (kushoto) akiwa na akiwa na Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi wa Tume hiyo Yusufu Rauna (kulia) wakiwa kwenye mkutano huo. Mkurugenzi wa Idara ya Ithibati kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Dkt. Kassile Telemu (kushoto) na Afisa Ithibati wa Tume hiyo Alexander Kamwela (kulia) wakiwa kwenye Mkutano huo uliofanyika kwenye Ofisi za Tume hiyo Jijini Dar es Salaam.
*********************************
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania imetangaza kufungiwa kwa Dirisha la udahili kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu kwa Mwaka wa Masomo 2021/2022.
Tume ya Vyuo vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kufunguliwa kwa dirisha la udahili kwa waombaji wa shahada ya kwanza katika Taasisi za Elimu ya juu kwa Mwaka wa Masomo 2021/2022.
Akizungumzia na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji TCU, Prof. Charles Kihampa amesema kuwa Dirisha hilo limefunguliwa rasmi leo Julai 12,2021 kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha Sita hivi karibuni nakwamba inatoa fursa kwa wanafunzi hao kuanza mapema mchakato wa kufanya Maombi kwenye vyuo na Taasisi za Elimu ya Juu.
Aidha amesema kuwa Maombi yote ya udahili wa kujiunga na Shahada ya kwanza utahusu Makundi matatu ambayo ni wenye sifa stahiki za kidato cha Sita, wenye sifa stahiki za Shahada (Ordinary Diploma), na wenye sifa stahiki za Cheti cha Awali (Foundation Certificate) ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
“Maombi yatumwe moja kwa moja kwenye vyuo ambavyo muombaji amevichagua na kuchagua programu za masomo anazozipenda. Mwongozo wa programu zilizoidhinishwa kudahili na vigezo stahiki” Amesema Prof. Kihampa
Aidha Prof. Kihampa amewataka wanafunzi wanaofanya udahili kujihepusha na watu wanaojifanya kuwa ni mawakala na kujaza fomu za makaratasi na kusisitiza kutuma Maombi moja kwa moja vyuoni kupitia mifumo ya kielektroniki iliyowekwa na vyuo husika.