Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania Mhe. Tulia Ackson akipata maelezo ya namna utabiri wa hali ya hewa unavyoandaliwa kuanzia ngazi za awali kutoka kwa Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri, TMA, Bw. Samwel Mbuya wakati alipotembelea ofisi za TMA, Kituo Kikuu cha Utabiri, Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Tarehe 09/07/2021.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania Mhe. Tulia Ackson akipata maelezo ya namna uchambuzi wa hali ya hewa unavyofanyika kwa njia ya modeli za kimahesabu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi wakati alipotembelea ofisi za TMA, Kituo Kikuu cha Utabiri, Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Tarehe 09/07/2021.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania Mhe. Tulia Ackson akijionea hindi utabiri wa hali ua hewa kila siku unavyorekodiwa katika studio za TMA kwa ajili ya kuruka katika vyombo mbalimbali vya habari nchini wakati alipotembelea ofisi za TMA, Kituo Kikuu cha Utabiri, Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Tarehe 09/07/2021.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania Mhe. Tulia Ackson akipata maelezo ya namna taarifa za hali ya hewa za muda mrefu zinavyohifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya sekta mbalimbali ikiwemo miradi ya kimkakati kutoka kwa Meneja wa Klimatolojia, TMA, Dkt. Hashim Ng’ongolo wakati alipotembelea ofisi za TMA, Makao Makuu, Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Tarehe 09/07/2021.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania Mhe. Tulia Ackson akipata maelezo ya namna utabiri wa hali ya hewa unavyoandaliwa kuanzia ngazi za awali kutoka kwa Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri, TMA, Bw. Samwel Mbuya wakati alipotembelea ofisi za TMA, Kituo Kikuu cha Utabiri, Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Tarehe 09/07/2021.
Dar es Salaam; Tarehe 09 Julai, 2021;
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (MB) ametoa wito kwa vyombo vya habari kutenga muda wa kutosha wa kurusha taarifa za hali ya hewa mara kwa mara ili kusaidia wananchi kuzipata kwa wakati na kuzitumia kwa ufanisi zaidi. Aidha, alieleza kuwa kutokana na muda wa habari ya hali ya hewa kuwa mfupi, taarifa zinatolewa kwa ujumla na kwa ufupi, kitu ambacho kinaweza kuathiri matumizi yake.
“Nitoe wito kwa vyombo vya habari kuangalia namna ambavyo watakuwa wanazitumia taarifa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na kuzitoa mara kwa mara ili kutusaidia sisi wananchi kujiandaa na kufanya maamuzi sahihi katika mipango yetu, tuangalie kama vyombo vingine vya habari vya mataifa ya nje, ukifungua kila wakati unaangalia hali ya hewa”Alisema Dkt. Tulia wakati alipotembelea Makao Makuu ya TMA.
Aliendelea kusema kuwa, alichojifunza katika ziara yake fupi katika ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, ni kuwa taarifa zipo, lakini kwa ajili ya muda mfupi basi Mamlaka inalazimika kuziweka katika huo muda mfupi.
Kwa upande mwingine, alito wito kwa wananchi kuitembelea Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ili kujifunza masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na namna taarifa za hali ya hewa zinavyochakatwa kitaalamu hadi kumfikia mtumiaji.
Imetolewa na;
KITENGO CHA UHUSIANO,
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA (TMA).