*******************************
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene ameruhusu askari Polisi kuanza kutumia nyumba za kisasa zenye uwezo wa kubeba familia zaidi ya 300 zilizopo katika eneo la Kunduchi na Mikocheni jijini Dar es salaam.
Waziri Simbachawene amesema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kikazi na kukagua Mradi wa nyumba za kisasa za makazi ya askari ambapo ameelekeza kutumika kwa nyumba hizo ambapo kutasaidia kupunguza uhaba wa nyumba za askari na kuleta ufanisi kwa askari wanapotekeleza majukumu yao ya kazi za Kipolisi.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema tangu kukamilika kwa mradi huo imepita miaka mitatu hadi sasa jambo ambalo linapelekea kuharibika kwa baadhi ya sehemu za nyumba hizo kwa kukosa matunzo kwa kutokutumiwa na askari wa Jeshi hilo.