Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mwanaidi Ali khamis akichanganya zege wakati aliposhiriki ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Itunundu iliyopo Kijiji cha Itunundu Tarafa ya Pawaga Wilaya Iringa ikiwa ni sehemu ya kuamsha ari ya wananchi kujitolea kujiletea maendeleo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mwanaidi Ali khamis akimwaga zege katika moja ya msingi wa madarasa wakati akishiriki ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Itunundu iliyopo Kijiji cha Itunundu Tarafa ya Pawaga Wilaya Iringa ikiwa ni sehemu ya kuamsha ari ya wananchi kujitolea kujiletea maendeleo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mwanaidi Ali khamis akizungumza na wanafunzi walimu wa Shule ya Msingi Itunundu na wananchi wa Kijiji cha Itunundu Tarafa ya Pawaga Wilaya Iringa aliposhiriki ujenzi wa Shule kijijini hapo.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
…………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, Iringa
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mwanaidi Ali khamis amewataka wanafunzi kujenga ujasiri na kutoa taarifa dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsi pale vinapojitokeza ili waweze kutimiza ndoto zao maishani.
Naibu Waziri Mwananidi ameyasema hayo wakati waliposhiriki ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Itunundu iliyopo Kijiji cha Itunundu Tarafa ya Pawaga Wilaya Iringa ikiwa ni sehemu ya kuamsha ari ya wananchi kujitolea kujiletea maendeleo.
Akizungumza na wananchi wakati wa zoezi hilo Naibu Waziri Mwanaidi amesema Serikali inatekelza Mioango mbalimbali inayohakikisha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinatokomezwa ikiwemo Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wa Mwaka 2017/2018-2021/2022.
Aidha Naibu Waziri Mwanaidi amewapongeza wananchi wa kijiji hicho kwa jitihaza zao za kuchangia katika miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo amesema Serikali kwa upande wake itahakikisha inatatua changamoto mbalimbali zinazokwamisha juhudi za maendeleo.
Ameongeza kuwa katika jitihada za kuunga Mkono juhudi za wananchi, Wizara ya Afya-Iadara Kuu ya Maendeleo ya Jamii imechangia mifuko thelathini ya saruji ikiwa ni mchango wake kwa maendeleo ya ujenzi wa miundombini shuleni hapo.
Akisoma taarifa ya ujenzi wa madarasa vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Itunundu Mtendaji wa Kata ya Itunundu, Emmanuel Ngabuji amemshukuru Naibu Waziri kwa kutembelea shule hiyo na kushiriki ujenzi wa madarasa hayo na kutoa hamasa kwa wadfau wengine kusaidia juhudi za Serikalim katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Ngabuji amesema kuwa Wakazi wa Pawaga wanashiriki katika katika shughuli mbalimbali za maendeleo na hatua ya Naibu waziri kuwatembelea imewaongezea ari na kuongeza morali wa kujitolea katika kuhakikisha wanapata maendeleo katika kijiji chao.
Awali Naibu Waziri Mwanaidi alitembelea shule za Msingi Kimande na Itunundu ambako ameshuhudia Mabaraza na Klabu za watoto zilizoundwa maalumu kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na vitndo mbalimbali vya ukatili wa kijinsia.