Mchezaji wa Yanga Tuisila Kisinda akimtoka beki wa Simba Hussein Zembwa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara,Yanga imeshinda bao moja bila.
Mshambuliaji wa Simba John Bocco akijaribu kuwatoka wachezaji wa Yanga ,Mukoko Tonombe na Fei Toto mechi ya Ligi Kuu bara Yanga imeibuka na ushindi wa bao moja bila.
Mshambuliaji wa Yanga Yacouba Songne akipasua ngome ya Simba mbele ya Beki Onyango na Tshabalala mechi iliyoisha kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao moja bila
************************
Na.Emmanuel Mbatilo,Dar es salaam.
Simba imeshindwa kutangazwa bingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara baada ya kukubali kichapo cha bao 1_0 dhidi ya Yanga Mechi iliyoshuhudiwa na Rais wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Shujaa wa Yanga leo ni Kiungo Mkabaji Zawadi Mauya dakika ya 12 kwa shuti kali lililomshinda Mlinda Mlango wa Simba Aishi Manula.
Hii ni mara ya pili kwa Yanga kupata ushindi mbele ya Rais wa Tanzania kwani Msimu uliopita Yanga walishinda Bao moja mbele ya Hayati DK.John Magufuli bao ambalo lilifungwa na Bernard Morrison ambaye yeye leo alikuwa Simba na leo mbele ya Rais Samia imekufa bao moja bila.
Ushindi wa Yanga unaifanya Simba kushindwa kutawazwa bingwa kwa sasa itabidi isubiri mechi nyingine ambapo itashuka Julai 7 uwanja wa Mkapa kucheza na KMC.
Licha ya Yanga kupata ushindi inabaki nafasi ya pili kwa kufikisha Pointi 70 huku Simba ikibaki na pointi 73 na Mechi nne mkononi na Yanga wamebakiza mbili.
Kwa sasa macho na masikio ya watani wa Jadi na mashabiki wao ni Julai 25,2021 uwanja wa Lake Tanganyika Mjini Kigoma watakapocheza Fainali ya Kombe la Azam Sport Federation maarufu kama FA cup.