Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea la Kimarekani (Peace Corps) Bibi. Stephanie Joseph de Goes katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea la Kimarekani (Peace Corps) Bibi. Stephanie Joseph de Goes katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea la Kimarekani (Peace Corps) Bibi. Stephanie Joseph de Goes akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine Ripoti ya Mwaka ya Shirika hilo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea la Kimarekani (Peace Corps) Bibi. Stephanie Joseph de Goes akiagana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine mara baada ya kumalizika kwa maongezi yao.
**************************
Na Mwandishi wetu, Dar
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea la Kimarekani (Peace Corps) Bibi. Stephanie Joseph de Goes kwa lengo la kujitambulisha na kuelezea maandalizi ya ujio wa wafanyakazi wa kujitolea wa Shirika hilo kutoka Marekani.
Bibi. Stephanie Joseph de Goes amemueleza Balozi Sokoine kuwa wafanyakazi hao wanatarajiwa kuwasili hapa nchi kwa ajili ya kufanya kazi katika maeneo mbalimbali yenye uhitaji.
Pamoja na Mambo mengine, Katibu MKuu Balozi Sokoine amemhakikishia Mkurugenzi Mkazi huyo ushirikiano na kwamba Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika Mashariki iko tayari kuratibu utendaji wa shirika hilo hapa nchini kwa kushirikiana na Wizara nyingine za Kisekta zinazoguswa kiutendaji na Shirika hilo kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.