Diwani wa Kata ya Buguruni Bw.Busolo Pazia akikagua timu za mpira wa Netiboli kabla ya kuanza mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Netiboli yalioandaliwa na Taasisi ya Furahika Education College jijini Dar es Salaam.
Timu za Netiboli ya Majumba 6 na Vatcan wakiwa uwanjani wakiminyana kuwania ushindi katika mchezo huo uliyochezwa katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kiziwi Buguruni jijini Dar es Salaam.
****************************
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Mashindano ya Mpira wa Netiboli kwa Wanawake yanayoshirikisha timu 26 yameanza kutimua vumbi katika viwanja vya Shule ya Msingi Kiziwi iliyopo Buguruni jijini Dar es Salaam.
Mashindano hayo yanadhaminiwa na Taasisi ya Furahika Education College yenye kauli mbiu Kazi Iendelee ambayo yana lengo ya kuibua vipaji pamoja kutambua mchango wa utendaji wa siku 100 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu.
Akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya Netiboli yaliondaliwa na Taasisi y Furahika Education Center, Diwani wa Kata ya Buguruni, Bw. Busolo Pazia, amesema kuwa lengo la kuunga mkono juhudi za Rais pamoja kuendelea kukuza na kuendeleza vipaji.
Bw. Pazia alikuwa anamwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala katika uzinduzi huo, amesema kuwa serikali itaendelea kutoa ushirikiano ili kufikia malengo yaliokusudiwa.
“Serikali itaendelea kukuza vipaji vya mpira wa netiboli kwa wanawake kwa kuanzisha mashindano mbalimbali jambo ambalo litasaidia kuibua na kukuza vipaji vya vijana”
Akizungumza kwa niaba ya Taasisi ya Furahika Education College, Bw. David Msuya, amesema kuwa katika mashindano hayo kuna timu 25 za netiboli kutoa Mkoa wa Dar es Salaam ambayo yameanza Juni 30, 2021 na kutarajia kumalizika Julia 1 mwaka huu.
Amesema kuwa katika mashindano kutakuwa na zawadi ya fedha kwa mshindi wa kwanza hadi ya watu.
Katibu wa Chama Cha Mpira wa Netiboli Mkoa wa Dar es Salaam (CHANETA) Bw. Joseph Stanslaus, amesema kuwa mwitikio katika mashindano ni mkubwa kutoka na timu nyingi zimeomba kushiriki.
Bw. Slanslaus amewaomba wadau mbalimbali wa michezo kujitokeza ili kuendelea kusaidia michezo katika nyanja mbalimbali.