Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Bw. Ladslaus Matindi akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Leaders leo mara wakati wa zoezi la kuchangia Damu kwa wahitaji mbaimbali ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu.
Wafanyakazi wa Shirika hilo zaidi wameungana na wadau mbalimbali wanaoshirikiana nao katika biashara ili kuchangia damu na kuokoa maisha ya watu.
Meneja Masoko wa Shirika la Ndege la ATCL Bi. Christina Tungaraza kushoto akiwa na Grace Magubo Afisa Masoko wa Shirika hilo wakati wa uchangiaji wa damu kwenye viwanja vya Leaders leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Tanzania ATCL Bw. Ladslaus Matindi akifurahia jambo na Meneja Masoko wa Shirika la Ndege la ATCL Bi. Christina Tungaraza mara baada ya kumalizika kwa Jogging tayari kwa ajili ya wadau kuanza zoezi la kuchangia damu kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa ATCL na wadau mbalimbali waliojitokeza kuchangia damu wakifanya Jogging leo asubuhi kabla ya kuanza kuchangia kwenye viwanja vya Leaders.
Baadhi ya washiriki wa mazoezi hayo ya Jogging na baadhi ya wafanyakazi wa ATCL wakifanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuanza kuchangia damu kwenye viwanja wa Leaders leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa ATCL na wadau mbalimbali wakijiandikisha kwa ajili ya kuchangia damu leo kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wadau wakichangia damu kwenye viwanja vya Leaders leo jijini Dar es salaam anayewahidumia ni Quicy Calvin Afisa kutoka Mpango Damu Salama.
Joel Nyembea Afisa kutoka Mpango wa Damu Salama akiwahudumia baadhi ya wadau waliokuwa wakijitolea damu leo kwenye viwanja vya Leaders.
Joel Nyembea Afisa kutoka Mpango wa Damu Salama akimhudumia Anne-Marie Sendiga Katibu wa Mkurugenzi Mtendaji (ATCL) wakati alipokuwa akichangia damu kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam leo.
Quicy Calvin akimhudumia Gloria Joseph Afisa Mwendeshaji wa Ndege (ATCL) wakati alipokuwa akichangia damu kwenye viwanja vya Leaders leo jijini Dar es salaam.