*****************************
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila amesema kuendeleza mafanikio yaliyofikiwa katika sekta ya elimu, Mkoa wa simiyu upo kati ya 10 bora kuanzia elimu ya msingi mpaka Sekondari hivyo ni vyema kulinda na kuendeleza mafanikio hayo.
Ameyasema hayo alipokuwa anamuapisha Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe.Lupakisyo Adrea Kapange katika Viwanja wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa – Bariadi Simiyu.
Amesema kuwa wakati Tanzania ni kinara wa kuzalisha Pamba Mashariki na Kusini ya Afrika, Simiyu inazalisha zaidi ya asilimia 55% ya pamba yote. Malengo ni kuongeza uzalishaji kufikia tani 500,000 msimu ujao kwa kuongeza usimamizi ili kuongeza tija.
“Tupo msimu wa mauzo ya pamba. Nilielekeza ma DC wote waende kukutana na Kamati za usalama wilaya na vikosi kazi vya kudhibiti michezo michafu dhidi ya wakulima kwenye mauzo, nimeshatangaza sintokuwa na huruma kwa yeyote anaehujumu jasho la mkulima”. Amesema RC.Kafulila.
Aidha RC.Kafulila amesema Sekta ya Afya inahitaji usimamizi wa ziada, CHMT zetu kuna uzembe mkubwa wa usimamizi hivyo amemtaka Mhe.Kapange kuhakikisha unaongeza uhai wa usimamizi wa sekta ya Afya kwenye wilaya yake.
“Kwa ulivyosema kwenye salamu zako Mhe. DC hakikisha unatumia sehemu kubwa ya muda wako walau asilimia 50% kuangalia utaboresha nini kwenye shughuli za watu kwenye maeneo mengi ili kuongeza tija katika shughuli zao na hivyo kipato chao”. Amesema RC.Kafulila.