WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk. Damas Ndumbaro,akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo June 25,2021 jijini Dodoma kuhusu kumsimamisha kazi Meneja wa shamba la hifadhi ya misitu la Silayo lililopo Bukombe mkoani Geita.
Naibu waziri Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja,akizungumza na waandishi wa habari leo June 25,2021 jijini Dodoma kuhusu kusimamishwa kazi kwa Meneja wa shamba la hifadhi ya misitu la Silayo lililopo Bukombe mkoani Geita.
……………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk. Damas Ndumbaro,amemsimamisha kazi Meneja wa shamba la hifadhi ya misitu la Silayo lililopo Bukombe mkoani Geita Bw.Thadeus Shirima, kwa kufanya oparesheni ya kuwaondoa watu bila kuwa na kibali.
Tamko hilo amelitoa leo June 25,2021 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari Dkt.Ndumbaro amesema kuwa kuwa Meneja huyo anasimamishwa ili kupisha uchunguzi juu tuhuma zinazomkabili.
”Tumemsimamisha kazi meneja huyo kufuatia malalamiko juu ya operesheni hiyo yaliyotolewa na wabunge wa majimbo yanayolizunguka shamba hilo wakiongozwa na Mbunge wa Bukombe Dotto Biteko kuwasilishwa Wizarani’amesema Dkt.Ndumbaro
Amesema kuwa hali hiyo imewasababishia wananchi hao kupoteza mali zao ikiwemo nyumba pamoja na mashamba.
Dkt.Ndumbaro amesema kuwa wizara hiyo imeamua kumsimamiasha kazi Meneja huyo na kumwagiza katibu mkuu kupeleka mtu mwinginwe atakaye kwenda kushika nafasi hiyo.
Dk. Ndumbaro amesema kuwa kitendo cha kujichukulia madaraka mikononi ambacho amefanya meneja huyo kinaharifu sura ya wizara hiyo pamoja na falsafa ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
“Oparesheni hii iliyofanywa bila kufuata utaratibu sisi wizara hatuwezi kuifumbia macho kabisa lazima yoyote aliyehusika katika hili tutamshugulikia”amesema
Hata hivyo ameelezea kuwa tayari wizara imeshapeleka timu ya wataalamu watakaofanya tathmini kwa muda wa wiki mbili na kuwasilisha ripoti itakayofanyiwa kazi.
Kwa upande wake Naibu waziri Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja,ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa watumishi hususani wa wizara hiyo kufanya kazi kwa kufuata sheria kanuni na taratibu na vinginevyo wataendelea kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria na kanuni za utumishi wa umma.