Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Dorothy Gwajima wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa sekta ya Afya awamu ya tano (HSSP V ,2021-2025) hafla iliyofanyika Leo June 24,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe.Stanslaus Nyongo,kizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa sekta ya Afya awamu ya tano (HSSP V ,2021-2025) hafla iliyofanyika Leo June 24,2021 jijini Dodoma.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani Dkt.Tigest Ketsela Mengestu,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa sekta ya Afya awamu ya tano (HSSP V ,2021-2025) hafla iliyofanyika Leo June 24,2021 jijini Dodoma.
Mwakilishi wa USAID Tanzania Andy Karas,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa sekta ya Afya awamu ya tano (HSSP V ,2021-2025) hafla iliyofanyika Leo June 24,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk. Ntuli Kapologwe,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa sekta ya Afya awamu ya tano (HSSP V ,2021-2025) hafla iliyofanyika Leo June 24,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa sekta ya Afya awamu ya tano (HSSP V ,2021-2025) hafla iliyofanyika Leo June 24,2021 jijini Dodoma
……………………………………………………………………………………..
Na Alex Sonna,Dodoma
SERIKALI imezindua Mpango Mkakati wa sekta ya Afya awamu ya tano (HSSP V ,2021-2025) huku ikitarajia kutumia kiasi shilingi trilioni 47 katika kipindi cha miaka mitano kwenye utekelezaji wa Mpango huo
Mpango huo upo katika maeneo matano ya kimkakati ikiwemo kuboresha utoaji huduma za afya kulingana na mahitaji zikiwemo huduma za afya ya mama na mtoto.
Akizungumza leo June 24,2021 wakati wa uzinduzi wa mpango huo,Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Doroth Gwajima amesema kwa kila mwaka zitatumika takribani shilingi trilioni 9.4 na kwamba kiasi hicho cha fedha kinatarajiwa kuokoa maisha ya wananchi 200,000 zaidi watakaofikiwa na huduma zilizoboreshwa .
Waziri Gwajima amesema wastani wa wati 400,000 watapona kwa kuwa na afya bora na kurejea katika shughuli za kimaendeleo kwa kupata huduma bora zitakazoboreshwa kupitia utekelezaji na tathim,ini na ufuatiliaji wa pamoja wa Mpango Mkakati huo.
Amesema katika kipindi miaka mitano iliyopoita sekya ya afya imepata mafanikio makubwa ikiwemo kujenga vituo vya kutolea huduma za afya 1,887 ,na katika miaka mitano ijayo Serikali ya awamu ya sita itaendeleza juhudi za kupunguza vifo vya wajawazito na watoto,kuboresha huduma za akina mama wajawazito.
Waziri huyo amesema katika eneo hilo pia itaboreshwa huduma ya afya ya vijana,afya ya jamii,Elimu ya afya,Lishe,usafi wa mazingira ,magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza,ambayo yanasababisha vifo vingi na kuigharimu Serikali fedha nyingi.
Amesema eneo lingine la kutiliwa mkazo kwenye utekelezaji wa mkakati huo ni kuimarisha utayari wa kujiandaa kukabiliana na magonjwa ya milipuko na magonjwa ya dharura huku akitolea mfano mlipuko wa covid -19.
Amesema hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan aliteua kamati maalum ya wataalm kumshauri na kutoa mapendekezo ya kukabiliana na ugonjwa wa Covid -19 hapa nchini.
Waziri huyo amesema kamati hiyo iliwasilisha taarifa na mpango kazi wa mapendekezo 19 yanayotakiwa kufanyiwa kazi na Serikali.
“Sasa nichukue fursa hii kuwafahamisha wizara ya Afya inaandaa andiko litakalowasilishwa kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri .”amesema Dkt.Gwajima
“Serikali ya Tanzania imeshaandaa andiko la kupata chanjo za ugoinjwa wa Covid -19 katika kukabiliana na wimbi la tatu la la mlipuko wa ugonjwa huo ,serikali kuanzia mwezi Julai mwaka huu itahusisha vikao vya kitaalam chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Serikali na Mwenyekiti Mwenza wa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani,”amesema
Dkt.Gwajima ameelekeza kufanyika vikao vya kila mhimili za Mpango wa Taifa wa Kudhibiti ugonjwa wa Covid -19 kwa lengo la kudhibiti ugonjwa huo hapa nchini.
“Katika utekelezaji wa mpango mkakati huo serikali itaendeleza jitihada za kuboresha kitita cha huduma za afya katika ngazi ya msingi na huduma za rufaa ,huduma za utengamano ,huduma za shufaa ,huduma za tiba asili na tiba mbadala,”amesema.
Waziri huyo amesema eneo jingine la kimkakati katika mpango huo kuwa ni kuimarisha uhusiano wenye matokeo chanya wa kiutendaji wa mifumo ya afya na kuendelea kuwekeza katika kuimarisha mifumo ya afya hususan katika rasilimali watu katika sekta ya afya ,dawa na bidhaa za afya kwa ujumla.
Hata hivyo,Waziri huyo ameiomba Wizara ya Fedha na Mipango kuendelea kuipa kipaumbele sekta ya afya kutoka kwenye vyanzo vya ndani huku akiwaomba washirika wa Maendeleo kuendelea kuchangia rasilimali fedha kwenye sekta ya afya kupitia bajeti kuu ya Serikali .
Vilevile, ameiasa sekta binafsi iendelee kuboresha mashirikiano katika utoaji huduma katika ngazi zote .
Akizungumza kwa niaba ya Wadau wa Maendeleo Andy Karas amesema ,mpango mkakati huo umekuja wakati muafaka huku akionyesha kufurahishwa na kaulimbiu ya mpango mkakati huo isemayo ‘mtu asiachwe nyuma’.
Amesema,kaulimbiu hiyo inafuatana na waraka wa dira ya Maendeleo ya Tanzania wa mwaka 2025 pamoja na waraka wa Malengo Makuu ya Taifa ya Maendeleo Endelevu Duniani ya Umoja wa Mataifa huku akisema nyaraka hizo zinalenga maendeleo Jumuishi yenye usawa ya kukidhi mahitaji na haki ya kimaendeleo.
“Mpango huu umefuatilia mwongozo wa Shirika la Afya Duniani ambao ni kuhakikisha maisha mazuri na imara kwa rika zote lakini pia unagusa vipaumbele vya nchi kama kupunguza vifo vya akina mama na watoto ,kupanua upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi na upangaji wa uzazi ,kutokomeza magonjwa ya kuambukiza kama ugonjwa wa ukimwi ,kifua kikuu ,malaria na homa ya ini,”amesema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe.Stanslaus Nyongo,amesema wao kama watunga sera watahakikisha hawaleti vikwazo katika utekelezaji wa mpango huo.