Home Mchanganyiko NAIBU WAZIRI SILINDE AGAWA VIFAA VYA MAABARA NA VIFAA SAIDIZI NCHINI ATOA...

NAIBU WAZIRI SILINDE AGAWA VIFAA VYA MAABARA NA VIFAA SAIDIZI NCHINI ATOA MAAGIZO MAZITO KWA MAKATIBU TAWALA

0

Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.David Silinde,akizungumza wakati wa zoezi la ugawaji wa vifaa vya Maabara kwa shule za sekondari na vifaa visaidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu hafla iliyofanyika leo June 24,2021 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu,Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dk.Leornad Akwilapo,akitoa neno wakati wa zoezi la ugawaji wa vifaa vya Maabara kwa shule za sekondari na vifaa visaidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu hafla iliyofanyika leo June 24,2021 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli,akizungumza wakati wa zoezi la ugawaji wa vifaa vya Maabara kwa shule za sekondari na vifaa visaidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu hafla iliyofanyika leo June 24,2021 jijini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.David Silinde,akipata maelezo kutoka kwa Mwanafunzi wa kidato cha nne Aboubakar Chaula  wakati wa zoezi la ugawaji wa vifaa vya Maabara kwa shule za sekondari na vifaa visaidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu hafla iliyofanyika leo June 24,2021 jijini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.David Silinde,akipata maelezo kutoka kwa Mwanafunzi wa kidato cha nne Pendo Masoud  wakati wa zoezi la ugawaji wa vifaa vya Maabara kwa shule za sekondari na vifaa visaidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu hafla iliyofanyika leo June 24,2021 jijini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.David Silinde,akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimba mara baada ya kuzindua  zoezi la ugawaji wa vifaa vya Maabara kwa shule za sekondari na vifaa visaidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu hafla iliyofanyika leo June 24,2021 jijini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.David Silinde,akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Dodoma Sekondari mara baada ya kuzindua  zoezi la ugawaji wa vifaa vya Maabara kwa shule za sekondari na vifaa visaidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu hafla iliyofanyika leo June 24,2021 jijini Dodoma.

………………………………………………………………….

Na Alex Sonna,Dodoma

SERIKALI imegawa na kusambaza  vifaa mbalimbali vya Maabara vyenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 3 kwa ajili ya shule 1,253 nchini ambavyo vitatumika katika maabara za Fizikia,Kemia na Biolojia huku ikiwataka Makatibu Tawala kuhakikisha vinapelekwa mpaka ngazi ya shule kabla ya Julai 15,2021.

Akizungumza leo,June 24,2021 wakati wa zoezi la ugawaji wa vifaa vya Maabara kwa shule za sekondari na vifaa visaidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu ,Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) David Silinde amesema Serikali ya awamu ya sita inaendelea na azma ya kuboresha utoaji wa elimu nchini katika kuimarisha sekta ya viwanda.

Amesema katika utekelezaji wa matamko ya kisera Tamisemi imefanya ununuzi wa vifaa mbalimbali vya kufundishia na kujifunzia hususan kwa masomo ya sayansi na wanafunzi wenye mahitaji maalum.

“Naomba nichukue fursa hii kuwaeleza kuwa Serikali imenunua vifaa mbalimbali vya maabara kwa ajili ya kuboresha ufundishaji na ujifunzaji katika shule za Sekondari.Serikali imenunua vifaa vyenye thamani ya shilingi,3,949,698,143,03,vifaa hivi vitakawanywa kwa shule za Sekondari 1,253 nchini na vitatumika katika maabara za Kemia,Fizikia na Biolojia,”amesema.

Naibu Waziri Silinde amesema huo ni utaratibu wa kawaida wa Serikali kuhakikisha kuwa nchi inapata wataalamu wa kada mbalimbali  wenye maarifa ya kutosha katika kuchangia kuimarisha uchumi wa Viwanda.

Hata hivyo,Naibu Waziri Silinde ametoa maagizo matatu kwa Makatibu Tawala wa Mikoa kwanza kuhakikisha vifaa hivyo  vinapelekwa mpaka ngazi ya shule kabla ya Julai 15,2021.

Pili,kuwasilisha taarifa ya mapokezi  na usambazaji wa vifaa hivyo  kwa Katibu Mkuu Tamisemi kabla au ufikapo tarehe 20 Julai 2021.

Tatu,kuhakikisha vifaa visaidizi kwa watu wenye ulemavu  vinafika na kugawanywa kwa wanafunzi wenye mahitaji kama ilivyobainishwa  kwenye taarifa ya awali ya tathmini ya hali ya wanafunzi hao.

Aidha,amesema Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imeandaa mkakati wa kitaifa wa elimu jumuishi wa mwaka 2018-2021 kwa lengo la kuboresha usimamizi na utoaji wa elimu kwa usawa na kwa makundi yote.

Naibu Waziri huyo amesema katikka hatua mbalimbali za utekelezaji Serikali imebaini wanafunzi wenye mahitaji maalum walikuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa vifaa visaidizi vya kujifunzia na kufundishia.

Amesema katika utekelezaji Serikali imenunua  vifaa visaidizi kwa ajili ya kununua makundi hayo vyenye thamani ya zaidi ya  shilingi bilioni moja.

“Ni katika utekelezaji wa maudhui ya matamko,sheria,sera na matamko mbalimbali yanayohusu utoaji wa elimu Serikali imenunua vifaa visaidizi kwa ajili ya kununua makundi hayo vyenye thamani ya shilingi 1,611,601,980,000,”amesema.

Amesema kundi la pili la vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum ni vifaa visaidizi vya kujifunzia darasani ambapo vitagawanywa katika shule 697 za msingi an sekondari ili kuweka mazingira rafiki kwa kundi hilo kujifunza wakiwa shuleni.

“Ofisi ya Rais Tamisemi inazindua ugawaji wa vifaa visaidizi kwa wanafunzi waliopo shule za msingi na sekondari wenye mahitaji maalum waliogawanywa kwenye makundi ya viziwi,wasioona,albino,wenye uoni hafifu,wenye ulemavu wa viungo wenye ulemavu wa akili wenye usonji na wenye uziwi na kutoona,”amesema.

Awali, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli, amesema vifaa saidizi vinapelekwa katika Halmashauri 65 zenye vitengo na shule za mahitaji maalum ambazo hazikupata vifaa hivyo katika ugawaji wa awamu ya kwanza.

Kwa upande wake,Katibu Mkuu,Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dk.Leornad Akwilapo,amesema kuwa vifaa hivyo vimegaiwa ili kutoa fursa ya kupata elimu kwa muda wote.