Mhe. David Kafulila mkuu wa mkoa wa Simiyu akiongea na madiwani.
Mwenyiti wa CCM mkoa wa Simiyu Bi. Shamsa Mohamed akiongea na madiwan
Wajumbe wa Baraza la Madiwani wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh.David Kafulila.
Viongozi wa Mkoa na Halmashauri ya Wilaya Maswa
…………………………………….
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulika leo amezungumza na kuwafunda madiwani, wakati alipohudhuria kikao cha Baraza Maaalum la Madiwani cha kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Serikali (CAG) kuhusu hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka 2019/2020 – Halmashauri ya Wilaya ya Maswa na Bariadi ambapo Vikao hivyo vilifanyika leo 23/6/2021 katika nyakati tofauti.
Mhe. Kafulila aliambatana na M/kiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Bi. Shamsa Mohamed na viongozi wengine wa Chama na Serikali.
Akizungumza na Baraza la Madiwani la Maswa, Bi. Shama aliwataka Madiwani hao kufanya kazi kwa ushirikiano na kusimamia miradi yao yote,vilevile alitumia wasaa huo kumfahamisha Mkuu wa Mkoa Kuhusu changamoto kubwa ambayo Madiwani wote wanakabiliana nayo ambayo ni posho kwa madiwani.
Akizungumza na Baraza hilo la Madiwani la Maswa ,Mkuu wa Mkoa,aliwakumbusha Madiwani hao kuwa wamechaguliwa na wananchi kwa kura nyingi, hii ikionyesha imani kubwa ambayo wananchi wanayo kwao, hivyo mnapaswa kuhakikisha kuwa mnaacha alama,ambayo ikakumbukwa milele hata baada ya kumalizia muda wenu.Wilaya ya Maswa ni kubwa kuliko hata baadi ya nchi kama Rwanda na Singapore.
Hivyo itendeeni haki Maswa. Pili, Wilaya ya Maswa ni wilaya iliyofanya vizuri sana katika mapinduzi ya Viwanda, mmeonyesha mfano mzuri sana wa mapinduzi yanayopaswa kulindwa.
Mmeanzisha baadhi ya viwanda na viwanda ni biashara, hivyo ni lazima hivi viwanda viendeshwe kibiashara na kwa faida. Changamoto ninayoiona hapa ni namna ya kuviendesha viwanda hivyo kwa faida.Viwanda hivyo vinapaswa kuwa chanzo cha mapato na sio chanzo cha matumizi.
Ili kulifanikisha hili tayari nimeshawasilaiana na Soko la Mitaji la Dar Es salaam (DSE) ambao wamekubali kuja Simiyu ili kubadilishana uzoefu na ikuona ni jinsi gani na nini kifanyike ili Viwanda hivi viwe endelevu.Soko la Mitaji ni muhimu sana kwa sababu viwanda vyote vinavyoendeshwa kupitia soko la Mitaji ndio viwanda vinavyoendelea kufanya vizuri hata baada ya kutaifishwa, mfano mzuri ni Taasisi kama vile TBL,NMB,TCC nk.
Kwa kuviingiza viwanda vyetu kwenye soko la mitaji tutavipatia fursa ya kuviongezea Mitaji na kuvifanya vifanye kazi kibiashara zaidi/corporate level.Pamoja na Mafanikio katika masuala ya elimu kimkoa, na uanzishwaji wa Viwanda Maswa, Mhe Mkuu wa Wilaya na Waheshimiwa Madiwani, bado kuna changamoto kubwa sana kwenye masuala ya Afya, CHMT ,hazifanyi kazi vizuri. Hivyo hakikisheni zinatimiza majukumu yao.
Tumieni nguvu kazi ya bei nafuu kama mgambo na Magereza kwani hii ni nguvu kazi yenye bei nafuu, watumieni kwenye baadhi ya maeneo, ili Kupunguza gharama.Niwapongeze kwa kupata hati safi,lakini pamoja na hati safi hiyo bado kuna maeneo kama manne ambayo, Mkurugenzi na Mkuu wa wilaya ya maswa nahitaji kupatiwa maelezo:
Eneo la kwanza, nina hitaji kupata maelezo ya kwanini deni la karibu 750m halijalipwa kwa zaidi ya mwaka?Halmashauri hazipaswi kulimbikiza madeni kiasi hiki kwani ni moja ya sababu ya wazabuni kutoa huduma kwa bei kubwa wakijua kwamba madeni yao hayalipwi kwa wakatiEneo la pili, nataka maelezo ni kwanini Halmashauri ilipeleka asilimia 22% ya fedha za ndani kwenye miradi ya maendeleo badala ya asilimia 40% kama maelekezo? Huu ni udhaifu mkubwa na sitaki kuona hali hii ikijirudia. Msukumo wa agenda hii ni mkubwa na ni moja ya kipimo cha DED kwenye nidhamu ya matumizi.
Tatu,nahitaji maelezo ya kina ni kwanini halmashauri ilitekeleza makisio ya makusanyo ya ndani kwa asilimia 39% , yaani chini ya nusu ya makisio kwa kukusanya 1.5bn badala ya 4bn ambayo ni lengo mlilojiwekea wenyewe
Nimeona kuwa Magari yenu mengi ni mabovu na haya tengenezeki, hivyo naelekeza Halmashauri yenu kuona uwezekano wa kufungua karakana yake yenyewe kwa ajili ya matengenezo ya magar, kama mlivyofanikiwa kuanzisha duka la Madawa/Pharmacy yenu ambayo ni kubwa na ya mfano, nina hakika mkianzisha karakana itasaidia sana na sio tu kama chanzo cha mapato lakini zaidi kuokoa fedha nyingi kwenye matengenezo ya magari kutokana na changamoto za kutafuta mafundi au kutumia Tasisi ambazo gharama zake ni kubwa sana Sitakubali Halmashauri inayofanya madhaifu katika ukusanyaji wa mapato.
Mkuu wa Wilaya hakikisha kila siku unajua POSs imekusanya kiasi gani, haiwezekani tuna kusanya 39% halafu tukajiona tupo vizuri,Akizungumza na Baraza la Madiwani Bariadi Mji , Mkuu wa Mkoa aliwafahamisha kuwa Ubora wa uchumi ndio unaoamua ukubwa wa eneo,mfano mzuri ni nchi ya ingapore ambayo ina ukubwa wa kilometa za mraba 740,lakini uchumi wake una thamani ya dola 370bln, sawa na thamani ya uchumi wa nchi zote za afika Mashariki, hivyo ukubwa wa maendeleo yetu unapimwa na sisi wenyewe.
Mkijipanga vizuri kuanzia Serikali za vijiji, Serikali za Mtaa na mji mtakuwa na mafanikio mazuri.
Elimu ndio inayobadilisha hatma ya watu,hivyo ongezeni jitihada nazidisheni agenda ya elimu, jueni kwamba ninaridhishwa sana na utendaji kazi wenu kielimu.
Eneo lenye changamoto ni idara ya afya CHMT, Ongezeni juhudi, sitaki tukasumbuane,badilikeni maana hamfanyi vizuri. Nimefarijika kusikia kwamba Zahanati 10 zinatumia mfumo na moja vifaa vyake vipo tayari.Wahudumieni wananchi kwa haki, msiwasumbue wala kuwanyanyasa wananchi,Mkurugenzi fuateni sheria,msionee watu.
Kasi ya kulipa Na kudai madeni iongezeke.Kutokana na Taarifa ya Mkaguzi wa Mahesabu ya serkali kwa mwaka wa fedha 2019/2020 natoa maelekezo yafuatayo; Halmashauri ya Bariadi kubadilika haraka katika utekelezaji hoja za CAG kwani ufanisi ni hafifu sana, kati ya hoja 24 zilizotilewa na hoja 19 bado hajafungwa hivyo nataka maelezo ya kina.Pili,Halmashauri inadai 3.5bn na kati ya hizo 2.4bn ni deni la zaidi ya mwaka.Udhaifu huu unachangia ufanisi duni wa halmashauri na hivyo nataka maelezo ya kina ndani ya siku mbili Tatu,Halmashauri inadaiwa zaidi ya 776m , deni la zaidi ya mwaka bila kulipwa.
Hii inachangia kuangusha biashara hasa za wazabuni wadogo. Nataka maelezo ya kina ndani ya siku mbiliNne,nataka kujua wafanyabiashara ambao halmashauri imeshindwa kuwatoza ushuru kiasi cha 41m ni kina na nani na kwanini.