………………………………………………………………….
Na Mathew Kwembe, Mtwara
Michuano ya UMISSETA inaendelea kushika kasi katika viwanja mbalimbali vya Chuo cha Ualimu na Shule ya Ufundi Mtwara kwa timu mbalimbali kujichukulia pointi muhimu dhidi ya wapinzani wao katika hatua ya makundi.
Matokeo ya michezo mbalimbali iliyopigwa leo inaonyesha timu za Unguja na Pemba ambazo nazo zinashiriki michuano hii hazijaja kinyonge kwani katika mpira wa wavu wavulana, unguja iliwafunga Pwani seti 3-0, na katika soka wavulana Pemba waliichapa Arusha magoli 2-0.
Matokeo mengine ya mpira wa wavu kwa wavulana yanaonyesha Dar es salaam waliwafunga Iringa seti 3-0, Tabora wameichapa Tanga seti 3-0, Mbeya wameifunga Rukwa seti 3-0, Mara dhidi ya Manyara 3-0, Ruvuma dhidi ya Singida 0-3, na Shinyanga dhidi ya Mtwara 2-3
Pia Lindi imeifunga Kagera seti 3-2, Simiyu wameichapa Pemba seti 3-0, Morogoro imefungwa na Njombe seti 1-3, Kilimanjaro imeifunga Songwe seti 3-0, Geita imeifunga Katavi seti 3-1, Songwe imefungwa na Shinyanga seti 0-3. Dar es salaam imeichapa Singida 3-1, na Simiyu imeifunga Pwani seti 3-1.
Mpira wa wavu wasichana Lindi imefungwa na Tabora seti 1-3, Simiyu imefungwa na Mbeya seti 0-3, Njombe imefungwa na Kilimanjaro seti 0-3, Mtwara imeichapa Ruvuma seti 3-0, Pemba ilichapwa na Morogoro seti 0-3, Dar es salaam imeichapa Kigoma setri 3-0, Manyara imefungwa na Mara seti 0-3, Ruvuma imefungwa na Tabora seti 0-3 na Morogoro imefungwa na Mbeya seti 0-3.
Kwa upande wa mpira wa kikapu katika michezo iliyochezwa leo katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara Shinyanga iliifunga Njombe vikapu 103-14, Kilimanjaro dhidi ya Simiyu 58-2, Rukwa dhidi ya Kigoma 30-17, Mtwara dhidi ya Dar es salaam 8-93, na Kilimanjaro dhidi ya Tabora 24-27.
Matokeo ya michezo mingine ya mpira wa kikapu yanaonyesha Mwanza imeifunga Ruvuma vikapu 43-16, Lindi dhidi ya Kagera matokeo 9-24, Arusha dhidi ya Dodoma 63-4, Mara dhidi ya Singida 7-39, Dar es salaam dhidi ya Ruvuma 104-12, Mbeya dhidi ya Mara 66-27 na Simiyu dhidi ya Singida 34-27.
Matokeo ya mchezo wa Netiboli hadi filimbi ya mwisho yanaonyesha Pwani 25 kagera 19, Njombe 20 Kigoma 23, Singida 37 Ruvuma 11, Songwe 44 Dodoma 15, Rukwa 20 Manyara 16, Arusha 17 Kilimanjaro 24, Katavi 24 Unguja 17.
Pia Iringa imefungwa na Tabora magoli 12-39, Lindi imechapwa na wenyeji Mtwara 17-23, Shinyanga imefungwa na Mbeya 18-21, Simiyu imeifunga Morogoro 23-21, na Mwanza imeifunga Kagera 42-7
Matokeo mengine ya mpira wa kikapu Lindi dhidi ya Kagera 9-24, Simiyu dhidi ya Singida 34-27, Mbeya dhidi Mara 66-27 na Dar es salaam dhidi ya Ruvuma 104-12.
Katika mpira wa kikapu wasichana timu ya mkoa wa Arusha imeifunga Dodoma 63-4 na Mara wamefungwa na Singida vikapu 7-39.
Kwa upande wa soka wavulana katika michezo iliyochezwa mchana katika viwanja mbalimbali vya chuo cha ualimu na shule ya ufundi Mtwara yanaonyesha Geita imeibugiza Pwani 5-2, Ruvuma na Mbeya 0-0, Simiyu imechapwa na Dar es salaam 0-2, Singida imeifunga Shinyanga magoli 2-0 na Dodoma imeichapa Morogoro 1-0.
Matokeo mengine ya soka wavulana Kilimanjaro ilifungwa na Tabora magoli 1-2, Mwanza ilichapwa na Tanga magoli 0-3, Katavi na Lindi 0-0, Unguja ilifungwa na Njombe 2-4, Songwe iliichapa Manyara magoli 2-0 na Mara ikaifunga Rukwa 1-0.
Michuano hiyo itaendelea tena hapo kesho katika viwanja mbalimbali vya Chuo cha Ualimu na Shule ya Ufundi Mtwara.