Home Mchanganyiko WCF YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA WAAJIRI KUWEKA MAZINGIRA MAZURI KAZINI ILI KUPUNGUZA...

WCF YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA WAAJIRI KUWEKA MAZINGIRA MAZURI KAZINI ILI KUPUNGUZA VIHATARISHI SEHEMU ZA KAZI

0

NA MWANDISHI WETU, MOROGORO

WAAJIRI kutoka sekta ya Umma na Binafsi mkoani Morogoro wameelezwa kuwa moja ya majukumu yao ni  kukuza mbinu za kuzuia ajali, magonjwa ama vifo vitokanavyo na kazi kwa kuzingatia sheria ya usalama na afya mahali pa kazi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidida kwa Wafanyakazi (WCF) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waajiri 165 wa mkoani Morogoro, Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini kutoka WCF Dkt. Abdulsalaam Omar alisema wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa waajiri wa mkoa huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Juni 22, 2021.

“Mfuko huu umeundwa kwa dhumuni la kukidhi matakwa ya mikataba ya kimataifa kuhusu fidia kwa wafanyakazi ambapo kukuza mbinu za kuzuia ajali, magonjwa ama vifo ni moja ya matakwa hayo.” Alifafanua Dkt. Omar

Aliwaambia washiriki kuwa Mfuko umekuwa na faida kubwa kwa wafanyakazi, waajiri na taifa kwa ujumla kwani wafanyakazi wana uhakika wa kinga ya kipato kutokana na majanga yasababishwayo na ajali, magonjwa au vifo vitokanavyo na kazi.

“Hali kadhalika waajiri nao wanapata muda zaidi wa kushughulikia masuala ya uzalishaji na uendelevu wa biashara zao kwani mfuko ndio unaobeba jukumu la kugharamia pindi mfanyakazi anapoumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi” alifafanua na kuongeza kuwa ‘Wafanyakazi nao wanapata utulivu kazini kutokana na kupungua kwa migogoro hasa pale ajali zinapotokea sehemu za kazi na hii inasaidia sana kuongeza tija na uzalishaji na kuchangia kuongeza pato la taifa.

Akiwasilisha mada kuhusu Usalama na Afya sehemu za kazi, Meneja Tathmini za Vihatarishi Sehemu za Kazi, Bi. Naanjela Msangi alisema ili kuzingatia sheria ya usalama na afya mahali pa kazi waajiri hawana budi kuweka mazingira mazuri ya kufanya kazi kwa kuwapatia wafanyakazi vifaa vya kujikinga (Protective gears) na wahakikishe wanavitumia ipasavyo.

Ili kuonyesha madhara ya kufanya kazi bila ya kuvaa vifaa vya kujilinda, Bi. Naanjela aliongoza washiriki kufanya onyesho la kuonyesha madhara kwa wafanyakazi kutokana na ajali  kazini. 

Wakizunguzma kwa nyakati tofauti baada ya kupata mafunzo hayo, washiriki walisema yamekuwa ni yenye manufaa makubwa kwao na bila shaka watatumia elimu waliyoipata ili kuhakikisha wanatekeleza vema jukumu la kuweka mazingira salama kwa wafanyakazi mahali pa kazi.

“Tusiridhike na tusibweteke na Mfuko kwa kusema midhali WCF ipo basi masuala ya usalama na afya mahali pa kazi iwe sio kipaumbele chetu la, tusifanye hivyo, Fidia iwe ni kitu cha mwisho ije pale tu inapohitajika. ‘hakuna  namna mtu akiumia au amepata ugonjwa basi aweze kupata fidia.” Alisema Iddi Fuko, Meneja wa Usalama Mahali pa Kazi, Unitrans Tanzania Limited, Morogoro.

Alisema mafunzo hayo yasibaki kwa washiriki tu bali yaende hadi kwa maofisa na wafanyakazi wa ngazi za chini ili elimu hiyo iweze kuwasaidia wengi.

“Mafunzo haya yamenipa motisha mkubwa kwa kutambua usalama kazini, lakini pia tumefundishwa umuhimu wa kulinda viungo vyetu na hivyo yatupasa kuweka mazingira mazuri mahali pa kazi ili kupunguza ajali na magonjwa kazini.” Alisema Dotto Ramadhani, kutoka Haki Hoteli Morogoro

Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini kutoka WCF Dkt. Abdulsalaam Omar (katikati) akiwa na Meneja Tathmini za Vihatarishi Sehemu za Kazi, Bi. Naanjela Msangi (kushoto) na Afisa Madai Mwandamizi, Bw. Silvanus Kuloshe, akizungumza wakati wa mafunzo ya siku moja kuwajengea uwezo waajiri mkoani Morogoro kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi na shughuli za Mfuko Juni 22, 2021.

Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini Mfuko wa Fidida kwa Wafanyakazi 9WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, akifungua mafunzo ya siku moja kuwajengea uwezo waajiri mkoani Morogoro umuhimu wa kuzingatia usalama na afya mahala pa kazi ili kupunguza vihatarishi sehemu za kazi. Mafunzo hayo yamefanyika Juni 22, 2021 mkoani Morogoro

Afisa wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bi. Neema Mushi (kulia), akimpatia mfuko wenye taarifa mbalimbali za WCF mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo wakati alipowasili ukumbini.
Afisa wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Mariam Lisasi (kulia) akimkaribisha mshiriki kuchukua nafasi ya kuketi
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa.

Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidida kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar (katikati) akiwa na Meneja Tathmini za Vihatarishi Sehemu za Kazi,
Bi. Naanjela Msangi (kushoto) na Afisa Mfawidhi Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Mkoani Morogoro Bw. Kasian Baraka tayari kuanza mafunzo hayo.
 

mmoja wa waajiri akizungumzia umuhimu wa kufaa vifaa vya kujikinga (protrctive gears) kwa wafanyakazi wakati wakitekeleza majukumu yao. Kulia ni Meneja Tathmini za Vihatarishi Sehemu za Kazi,
Bi. Naanjela Msangi 
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa.
Afisa Mwandamizi wa Afya na Usalama mahala pa kazi, Mfuko wa Fidida kwa Wafanyakazi, Bi. Tumaini Kyando (kushoto) akizunguzma wakati wa mafunzo ya siku moja kuwajengea uwezo waajiri mkoani Morogoro kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi. Kulia ni Meneja Tathmini za Vihatarishi Sehemu za Kazi,
Bi. Naanjela Msangi