Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, Baraka Ladislaus akibonyeza kitufe ili kumpata mshindi wa mwisho wa promosheni ya Bonge la Mpango ambapo Abdallah Mohamed Abdallah aliibuka mshindi na kuondoka na Toyota Fortuner, mpya, akishuhudia ni Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Elibariki Sengasenga (kushoto), Maafisa wa NMB pamoja na wateja wa benki hiyo.
Wafanyakazi wa NMB wakifurahia baada ya kupatikana mshindi wa promosheni ya Bonge la Mpango – Abdallah Mohamed Abdallah, mkazi wa Morogoro vijijini aliyejshindia Toyota Fortuner, baada ya droo ya mwisho kuchezeshwa Sengerema mkoani Mwanza, akishuhudia ni msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Elibariki Sengasenga.
*************************
Abdallah Mohamed Abdallah, mfanyabiashara na mkazi wa Morogoro vijijini ameshida zawadi ya gari mpya aina ya Toyota Fortuner yenye thamani ya sh. milioni 169 katika droo ya mwisho ya kampeni ya NMB Bonge la Mpango iliyochezeshwa mjini Sengerema Mkoani Mwanza.
Akizungumza wakati wa droo hiyo mbele ya Msimamizi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha, Elibariki Sengasenga, Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, Ladislaus Baraka alisema ushindi wa Abdallah umekamilisha orodha ya washindi 148 waliojishindia zawadi mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya Sh550 milioni tangu droo hiyo ilipozinduliwa mwezi Februari mwaka huu.
Kupitia kampeni hii, benki ya NMB imetoa zawadi ya fedha taslimu kwa washindi 120, pikipiki ya mizigo ya miguu mitatu aina ya LIFAN 24, magari matatu ya mizigo aina ya Tata ACE maarufu kama kirikuu na gari la kifahari aina ya Toyota Fortuner.
Akizungumza kwa njia ya simu baada ya kujishindia gari, Abdallah aliishukuru benki ya NMB kwa zawadi hiyo huku akiwahimiza watanzania kujenga utamaduni wa kuhifadhi fedha zao katika benki ya NMB. Alikiri kwani tangu aanze kuweka fedha NMB – ambayo ina matawi zaidi ya 225 nchini na machine za ATM zaidi ya 700 bila kusahau mawakala walitapakaa kila mahali, hajawahi kujuta kwani amekuwa mnufaika mkubwa wa huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo, na sasa amejishindia zawadi kubwa ya gari ambayo hakuitarajia.
“Bado sijaamini kama kweli nimeshinda zawadi ya gari kwa sababu hata sikujua kama kuna droo inachezeshwa leo; sina mengi zaidi ya kuishukuru NMB kwa zawadi hii,” alisema Abdallah.