Home Mchanganyiko MKUU WA MKOA WA RUVUMA AWAAPISHWA WAKUU WAPYA WA WILAYA

MKUU WA MKOA WA RUVUMA AWAAPISHWA WAKUU WAPYA WA WILAYA

0

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Kanali Laban Elias Thomas akiapishwa na mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma mjini Songea

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akimkabidhi mkuu wa wilaya ya namtumbo Dkt.Julius Keneth Ningu ilani ya CCM na kadi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuapishwa.

Baadhi ya wageni waalikwa wa,kishuhudia kuapishwa kwa wakuu wa wilaya wapya mkoani Ruvuma.

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Kanali Laban Elias Thomas akikabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ilani ya CCM na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuapishwa.

**************************

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amewaapisha Wakuu wa Wilaya wapya,  nakutoa maelekezo katika utendaji kazi wao.

Hafla  ya kuwaapisha Wakuu wa Wilaya imefanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu  wa Mkoa wa Ruvuma mjini Songea, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali.

RC Ibuge amewaagiza Wakuu wa Wilaya wahakikishe wanasimamia wananchi kushiriki katika masuala ya Ulinzi na Usalama katika maeneo yao,  kwa sababu hakuna maendeleo bila kuwa Ulinzi na Usalama.

“kasimamieni maendeleo ya kiuchumi na kijamii, hakikisheni  Miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yenu, inakuwa yenye tija na kukamilika kwa wakati”. alisisitiza RC Ibuge.

Maagizo mengine aliyoyatoa Mkuu wa Mkoa kwa Wakuu wa Wilaya ni kuhakikisha thamani ya fedha katika Miradi inaonekana, kuhakikisha uwepo wa   matumizi sahihi ya miradi iliwekezwa na Serikali na kuondoa na vikwazo katika ufanyaji biashara na kuhakikisha huduma zinapatikana kwa wakati na haraka.

RC Ibuge pia amewaagiza Wakuu wa Wilaya  kusimamia uwezeshaji wa Makundi maalum, ambayo ni wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, kwa kuhakikisha asilimia 10 ya fedha ya mapato ya ndani, inatengwa kwa ajili ya kundi hilo.

Mkuu wa Mkoa amewataka Wakuu wa Wilaya katika maeneo yao wakahamasishe wananchi kujiunga na Bima ya Afya iliyoboreshwa, na kuhakikisha Fedha inayotakiwa kununuliwa madawa inawekwa benki.

Amesisitiza kuhakikisha Mazao ya kimkakati  Soya, Ufuta, Mbaazi, Choroko na Korosho Kuuzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani, ili wakulima watimize ndoto zao, Pamoja  na kusimamia utekelezaji wa miradi inayotekelezwa na Taasisi za Umma zilizopo katika Halmashauri.

Ibuge amewaagiza Wakuu wa Wilaya  kutatua kero za wananchi, na kusimamia ukusanyaji wa mapato na matumizi sahihi ya fedha za umma, kusimamia masuala ya elimu, na matumizi bora ya pembejeo za kilimo na elimu ya biashara na ujasiliamali kwa ajili ya kuboresha kipato kwa wananchi.

Kwa upande wake  Mkuu Mpya wa Wilaya  ya Nyasa Kanali  Laban Thomas akizungumza baada ya kuapishwa, amehaidi kuwa Mtumishi, na kutokuwa mtawala  na kujifunza kutoka kwa wananchi pamoja na kuchukua changamoto zao na kuzifanya kuwa fursa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Julius Ningu ameahidi kushughulikia changamoto zinazowakabili wanachi wa Namtumbo na anatarajia kujifunza mengi kutoka kwa wananchi wenyewe.

Mkoa wa Ruvuma una wilaya tano ambazo ni Songea, Tunduru, Namtumbo,Mbinga na Nyasa.

Imeandaliwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Juni 22,2021