Home Mchanganyiko SERIKALI YASIKIA  KILIO CHA WANANCHI KUHUSU BILI ZA MAJI

SERIKALI YASIKIA  KILIO CHA WANANCHI KUHUSU BILI ZA MAJI

0

Katibu  Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga,akizungumza wakati akifungua kikao cha ushirikiano baina ya Wizara za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zenye dhamana ya sekta ya maji kilichofanyika leo June 21,2021 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji,Nishati na Madini Zanzibar Dkt .Mngereza Mzee Miraji,akizungumza wakati wa kikao cha ushirikiano baina ya Wizara za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zenye dhamana ya sekta ya maji kilichofanyika leo June 21,2021 jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa kikao wakifatilia hotuba ya Katibu  Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (hayupo pichani) wakati kikao cha ushirikiano baina ya Wizara za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zenye dhamana ya sekta ya maji kilichofanyika leo June 21,2021 jijini Dodoma.

Afisa Maendeleo ya jamii kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi.Zanipha Msangi,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki kwa Katibu  Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga mara baada ya kufungua kikao cha ushirikiano baina ya Wizara za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zenye dhamana ya sekta ya maji kilichofanyika leo June 21,2021 jijini Dodoma.

Katibu  Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua kikao cha ushirikiano baina ya Wizara za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zenye dhamana ya sekta ya maji kilichofanyika leo June 21,2021 jijini Dodoma.

…………………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

SERIKALI imesema mfumo wa Mita za Malipo Kabla ya Matumizi (LUKU) kwa wateja maji unatarajia kuanza mwezi ujao ambapo utasaidia kuondoa malalamiko ya wananchi kubambikiwa ankara za maji.

Hayo yameelezwa leo June 21,2021 na Katibu  Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga, wakati akifungua kikao cha ushirikiano baina ya Wizara za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zenye dhamana ya sekta ya maji.

Mhandisi Sanga amesema kuwa wanafikiria kuanza kutumia mita za kulipa kabla ya matumizi ambapo katika maandalizi hayo wanategenmea ndani ya wiki mbili maandalizi yatakuwa yamekamilika ambapo kuanzia Julai wataanza kufunga rasmi kwa wateja.

“Changamoto ambayo kwa sasa tunakumbana nayo ni malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu kubambikiziwa ankara za maji, mfumo huu wa kufunga mita za LUKU kabla ya matumizi umependwa na watu wengi kwa sababu mteja atalipa kwanza halafu ndio anapata huduma,” amesema

Aidha,Mhandisi Sanga amesisitiza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kuanza kutenga maeneo kwa ajili ya kuhifadhi maji taka ambapo sasa ni asilimia 30 ya maji  taka ndio yanayohifadhiwa.

Amesema itakuwa haina maana yoyote kama nguvu kubwa kuwekwa katika maji safi halafu wakasahau  namna ya kuhifadhi maji taka, kwani utafiti unaonyesha kuwa ukipeleka maji asilimia 80 kati ya hizo 40 yatakuwa maji taka.

“Katika hili nasisisitiza suala zima la kutafuta maeneo kote Tanzania Bara na Zanzibar kwa sababu miradi ya maji safi inahitaji sana maeneo, hivyo tusipokuwa makini tutajenga miradi ya maji safi lakini tusipoweka mikakati ya kuondoa maji taka itakuwa ni shida,”amesema Katibu Mkuu huyo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Maji,Nishati na Madini Zanzibar Dkt .Mngereza Mzee Miraji, amesema ushirikiano katika sekta ya maji  ni jambo zuri kwa sababu itasaidia kuboresha utendajikazi miongoni mwao.

“Ndoto ya ushirikiano ilikuwepo tangu miaka ya 50 iliyopita na sasa imetimia kwa vitendo.Wizara ya Maji na Madini kutoka Zanzibar tumepokea kwa mikono miwili suala la ushirikiano wa kisekta na Tanzania Bara, tunaamini ushirikiano huu utazaa matunda kwa wananchi wa pande zote mbili,”amesema..

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba, amesema sekta ya maji imeendelea kufanya vizuri kutokana na ushirikiano uliopo baina ya viongozi wote katika sekta hiyo.

“Ukweli miongoni mwa sekta ambazo zinafanya vizuri hapa Tanzania Bara huwezi kuacha kuongelea sekta ya maji, imekuwa bora sana, tuendelee kushirikiana miongoni mwetu,” amesema.