Home Mchanganyiko WAHIFADHI MISITU 79 TFS WASTAAFU KWA KUTEMBELEA USHOROBA

WAHIFADHI MISITU 79 TFS WASTAAFU KWA KUTEMBELEA USHOROBA

0

…………………………………………………………………………

Na MWANDISHI WETU

 KAMISHNA a wa Uhifadhi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS, Profesa  Dos Santos Silayo,  amewahakikishia wahifaadhi wastaafu kuwa Wakala utaendelea kushirikiana nao katika masuala mbalimbali licha ya kuwa wamemaliza muda wao wa kazi. 

Akizungumza jijini Dar es Salaam  mwishoni mwa wiki,katika hafla ya kuwaaga wahifadhi 79 waliostaafu katika mwaka huu wa fedha 2020/2021, alisema utumishi uliotukuka wa wahifadhi hao umesaidia kuleta ufanisi ndani ya TFS.

 “Napenda  kuwahakikishia kuwa Wakala utaendelea kuwa pamoja nanyi katika hali zote,” alisema Profesa Silayo.

 Kutokana na hali hiyo aliwataka wahifadhi wastafu hao kutosita kushiriki katika shughuli mbalimbali za TFS ili kuendeleza maboresho ya utendaji wa wakala huo na  kufikia malengo yake kupitia mpango mkakati wake. 

Kwa upande wake, Naibu Kamishna wa Uhifadhi wa  TFS, Emanuel Wilfred,  alisema tukio hilo ni la kihistoria kwa Wakala kwani tangu kuanzishwa kwake miaka 10, kwa mara ya kwanza wastaafu wameagwa kwa kwa pamoja. 

Alisema, TFS kwa  kutambua mchanga wa wastaafu hao wakiwamo  watumishi, imeamua kuwatunuku zawadi za fedha ambapo wastafu 59 kati ya 79 wamepewa sh.milioni 1.0  kila mmoja na  wastafu 16 wamepewa sh. milioni mbili kila mmoja, huku wawili wakipewa sh. milioni tatu na wengine wawili wakipewa sh. milioni 4. 

Naibu Kamishna huyo aliongeza kuwa fedha hizo zimetolewa kwa mujibu wa taratibu na vigezo zilizowekwa na mwongozo wa mkono wa pongezi wa TFS. 

Kwa upande wake Naibu Kamishna wa TFS aliyekuwa Kurugenzi ya Rasilimali Misitu,  Zawadi Mbwambo, aliushukuru uongozi wa wakala huo  kwa niaba yawastafu wote na kuahidi kuwa licha ya kstaafu bado  watakuwa sehemu ya familia  ya  TFS. 

Aliwataka watumishi wa wakala  huo ambao bado wapo kazini kufanya kazi kwa bidii na kupenda kazi zao na kuhakikisha kila mmoja hawi kikwazo cha mwenzie kutostaafu.

 “Nwasihi  watumishi mnaobaki hasa nyie mliobakiza muda mfupi,  miaka kuanza 10 kushuka chini, muda umekwisha mjiandae kustafu, hakuna cha kuogopa, maisha yatakwenda vizuri, lakini kwa wengine mliobaki hakikisheni hamuwi  sababu ya wenzenu  kutostafu,”  alisema Mbwambo.

Awali wastaafu hao walitembele Msitu wa Hifadhi Asilia wa Pugu Kazimzumbwi uliopo Kisarawe mkoani Pwani na kufanya shughuli za utalii