Home Mchanganyiko KATAMBI AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA BABA DUNIANI TANZANIA, NACOPHA YASHIRIKI

KATAMBI AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA BABA DUNIANI TANZANIA, NACOPHA YASHIRIKI

0

 

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akizungumza huku amebeba mtoto mgongoni ikiwa ni ishara ya kuunga mkono shughuli zinazofanywa na wanawake katika familia kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021.
 
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog 

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira),
Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini
ameongoza Maadhimisho ya Siku ya Baba Duniani ‘Father’s Day’ kitaifa ambapo kwa
mara ya kwanza yamefanyika nchini Tanzania katika mkoa wa Shinyanga.

Maadhimisho ya Siku ya Baba Duniani nchini Tanzania
yamefanyika leo Jumapili Juni 20,2021 yamefanyika katika Uwanja wa Zimamoto
Mjini Shinyanga  yakiongozwa na Kauli
Mbiu ‘Tembea katika viatu vyake, thamini mapambano yake’.

Maadhimisho hayo ya Siku ya Baba Duniani yenye lengo la
kusherehekea michango ya baba kwenye maisha ya watoto na familia kwa ujumla
yaliyoanza mwaka 1910 nchini Marekani yameandaliwa na Serikali kwa kushirikiana
na wadau likiwemo Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) na ICS Africa.

Katika maadhimisho hayo, wababa wameonesha kwa vitendo
baadhi ya shughuli zinazofanywa na wanawake ili kuonesha namna baba bora
anavyoshirikiana na mke wake katika majukumu ya matunzo,malezi na makuzi ya
familia na watoto. Pia kumefanyika zoezi la kuchangia damu salama na kupima
afya huku maandamano na burudani mbalimbali zikinogesha maadhimisho.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Naibu Waziri Ofisi
ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi amesema mkoa wa
Shinyanga umeamua kutumia siku ya Baba Duniani kuwapa wanaume nafasi  ya kutumia katika kulinda usalama wa wanawake
na watoto dhidi ya ukatili wa kijinsia kama watetezi wa haki za binadamu na
walinzi wakuu wa familia na jamii.

“Lengo la siku hii ni kuwafanya wanaume kuwa mstari wa mbele
katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia,maadhimisho haya yamekusudia
kutambua mchango wa wababa kama viongozi wa familia kwa kuwa wana wajibu mkubwa
wa kulinda, kutunza,kuongoza na kustawisha familia katika Nyanja za
kijamii,kielimu,kiuchumi na kiroho”
,ameongeza Katambi.

Amesema maadhimisho ya siku ya Baba duniani yatakuwa chachu
kwa wababa wa mkoa wa Shinyanga na Tanzania kwa ujumla katika kupinga ukatili
dhidi ya wanawake na watoto lakini pia kutambua mchango wa baba bora, baba
anayejali na kuheshimu utu wa wanawake, wasichana na watoto.

Katika hatua nyingine, Katambi ametumia fursa hiyo
kulipongeza Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA)  kwa kuwa mstari wa mbele katika shughuli za
mwitikio wa UKIMWI sambamba na kupinga vitendo vya unyanyapaa dhidi ya watu
wanaoishi na VVU pamoja na kutetea maslahi ya watu wanaoishi na VVU nchini.

“Ni dhambi na ni marufuku kumcheka na kunyanyapaa watu
wanaoishi na maambukizi ya VVU ama mtu mwenye ulemavu kwani hakuna ajuaye kesho
yake. Waliopata maambukizi hawakupenda. Tupendane, tuwe wamoja na tushirikiane.
Naomba wanaume tuwe mstari wa mbele kupima afya zetu na tukibainika tumepata
maambukizi basi tuanze kupata huduma ya dawa”
,amesema Katambi.

Katambi amewataka wababa kutambua changamoto wanazopitia
wake zao na kuwathamini hivyo kutoa wito kwa wababa wote kuwa mstari wa mbele
katika kuhakikisha wanashirikiana na wake zao katika majukumu mbalimbali ili
kujenga familia na jamii bora zaidi.

“Maadhimisho haya yawe sehemu ya mabadiliko makubwa katika
jamii yetu na kuondoa dhana potofu ya mfumo dume unaokandamiza makundi mengine
wakiwemo wanawake na watoto. Sisi wababa ni walinzi na wafariji wakuu wa
wanawake hivyo ni vyema tuwatunze, tuwapende na tuwaendeleze wake wake zetu”
,amesema
Katambi.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta
Mboneko akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Dkt. Philemon Sengati
amewataka wanaume kuwa mstari wa mbele kutetea haki za wanawake na watoto kwa
kuepuka ukatili wa kijinsia n unyanyasaji wa wanawake na watoto ambao hupelekea
majeraha makubwa ikiwa ni pamoja na ulemavu wa kudumu na kupoteza uhai.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu
wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA), Leticia Mourice Kapela amesema
NACOPHA inasherehekea siku ya baba duniani kwa kuelekeza nguvu na mtazamo wa
baba katika kuijenga na kuilinda familia ambayo ndani yake yumo mama au mtoto
anayeishi na maambukizi ya VVU.

“Tunasherehekea kwa kumuangalia baba ambaye anaishi na mama
au watoto ambao wanaendelea kupata huduma za UKIMWI zinazotolewa na serikali.
Thamani na utashi wa baba katika kumlinda mama na mtoto anayeishi na maambukizi
ya VVU ni jambo la msingi sana ambalo sisi NACOPHA tunalipigania kwa nguvu zote
na wakati wote”,
amesema Leticia.

“Hivi karibuni kumekuwa na matukio ya kikatili ikiwemo mauaji
ya akina mama ambao wanatumia dawa za ARV. Hii inadhihirisha wazi   kwamba
pamoja na juhudi za serikali na wadau kupinga na kuondosha unyanyapaa, ubaguzi
na matendo ya ukatili, matukio haya bado yapo hasa kwa watu wanaoishi na
maambukizi ya VVU. Matukio haya yanachangia kuchelewesha juhudi za serikali
kuzifikia 95-95-95”
,amesema.

Ameeleza kuwa baadhi ya matukio ya ukatili yanaunganishwa na
mila na desturi zisizofaa hivyo amehimiza viongozi wa jadi na dini kubeba
jukumu la kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuachana na mila na desturi
zinazowaumiza wanawake na watoto sambamba na kuhimiza wanaume kupima afya
zao,kulinda akina mama na watoto wanaotumia
huduma za UKIMWI.

Aidha ameshauri akina mama na watoto kutoa taarifa kwa
vyombo husika pale matukio  ya ukatili yanapotaka
kujitokeza au yanapotokea na serikali iendelee kuwashirikisha na kuwawezesha
watu wanaoishi na maambukizi ya VVU katika kuandaa mikakati ya kupambana na
ukatili wa kijinsia, kuendelea kufanya mapitio na maboresho ya sera,miongozo na
sheria mbalimbali ili ziwe chachu na kuelekeza wadau kukabiliana na unyanyapaa
na ukatili wa kijinsia.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akizungumza huku amebeba mtoto mgongoni ikiwa ni ishara ya kuunga mkono shughuli zinazofanywa na wanawake katika familia  kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021 kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akizungumza huku amebeba mtoto mgongoni ikiwa ni ishara ya kuunga mkono shughuli zinazofanywa na wanawake katika familia  kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA), Leticia Mourice Kapela akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akiteta jambo na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA), Leticia Mourice Kapela (kulia) , Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021.
Wanaume washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wakiandamana kutoka Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga kuelekea kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Wanaume washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe na vyombo wakiandamana kutoka Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga kuelekea kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga wakiwa kuni na ndoo za maji wakiandamana kutoka Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga kuelekea kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Waendesha bodaboda wakiwasili kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga wakati wa maandamano.
Washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga wakiwa wakionesha mabango yenye ujumbe mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini katika uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Wababa wakipita mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini wakiwa wamebeba kuni, ndoo za maji na watoto katika uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Vijana wa skauti wakionesha mabango yenye ujumbe mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini katika uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Mcheza ngoma ya Kisukuma maarufu Bugoyangi, bwana Mahona  kutoka kijiji cha Bugimbagu Shinyanga akimuweka kwenye suruali yake nyoka anayejulikana kwa jina la Nderema kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga
Wananchi wakimshuhudia Mcheza ngoma ya Kisukuma maarufu Bugoyangi, bwana Mahona  kutoka kijiji cha Bugimbagu Shinyanga akicheza na nyoka kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga
Mchezo wa Igizo kutoka Kikundi cha Sanaa ya Maigizo VIWAWASHI kinachopatikana Mkoani Shinyanga ukiendelea kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga
Akina baba wakiwa wamebeba watoto mgongoni kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali kupitia NACOPHA kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021 kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali kupitia NACOPHA kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021 kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali  kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021 kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akiwa katika banda la kuchangia damu salama kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021 kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021 kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021 kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021 kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021 kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021 kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021 kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
 
Picha zote na Kadama Malunde -Malunde 1 blog