…………………………………………………………………………
Na MWANDISHI WETU
KAMISHNA a wa Uhifadhi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS, Profesa Dos Santos Silayo, amewahakikishia wahifaadhi wastaafu kuwa Wakala utaendelea kushirikiana nao katika masuala mbalimbali licha ya kuwa wamemaliza muda wao wa kazi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki,katika hafla ya kuwaaga wahifadhi 79 waliostaafu katika mwaka huu wa fedha 2020/2021, alisema utumishi uliotukuka wa wahifadhi hao umesaidia kuleta ufanisi ndani ya TFS.
“Napenda kuwahakikishia kuwa Wakala utaendelea kuwa pamoja nanyi katika hali zote,” alisema Profesa Silayo.
Kutokana na hali hiyo aliwataka wahifadhi wastafu hao kutosita kushiriki katika shughuli mbalimbali za TFS ili kuendeleza maboresho ya utendaji wa wakala huo na kufikia malengo yake kupitia mpango mkakati wake.
Kwa upande wake, Naibu Kamishna wa Uhifadhi wa TFS, Emanuel Wilfred, alisema tukio hilo ni la kihistoria kwa Wakala kwani tangu kuanzishwa kwake miaka 10, kwa mara ya kwanza wastaafu wameagwa kwa kwa pamoja.
Alisema, TFS kwa kutambua mchanga wa wastaafu hao wakiwamo watumishi, imeamua kuwatunuku zawadi za fedha ambapo wastafu 59 kati ya 79 wamepewa sh.milioni 1.0 kila mmoja na wastafu 16 wamepewa sh. milioni mbili kila mmoja, huku wawili wakipewa sh. milioni tatu na wengine wawili wakipewa sh. milioni 4.
Naibu Kamishna huyo aliongeza kuwa fedha hizo zimetolewa kwa mujibu wa taratibu na vigezo zilizowekwa na mwongozo wa mkono wa pongezi wa TFS.
Kwa upande wake Naibu Kamishna wa TFS aliyekuwa Kurugenzi ya Rasilimali Misitu, Zawadi Mbwambo, aliushukuru uongozi wa wakala huo kwa niaba yawastafu wote na kuahidi kuwa licha ya kstaafu bado watakuwa sehemu ya familia ya TFS.
Aliwataka watumishi wa wakala huo ambao bado wapo kazini kufanya kazi kwa bidii na kupenda kazi zao na kuhakikisha kila mmoja hawi kikwazo cha mwenzie kutostaafu.
“Nwasihi watumishi mnaobaki hasa nyie mliobakiza muda mfupi, miaka kuanza 10 kushuka chini, muda umekwisha mjiandae kustafu, hakuna cha kuogopa, maisha yatakwenda vizuri, lakini kwa wengine mliobaki hakikisheni hamuwi sababu ya wenzenu kutostafu,” alisema Mbwambo.
Awali wastaafu hao walitembele Msitu wa Hifadhi Asilia wa Pugu Kazimzumbwi uliopo Kisarawe mkoani Pwani na kufanya shughuli za utalii