*********************************
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa ameagiza Chama cha Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano wa Serikali kusimamia utekelezaji wa Maazimio ya Kikao kazi kilichofanyika hivi karibuni Jijini Mbeya.
Mhe. Bashungwa ametoa agizo hilo leo Juni 17, 2021 Jijini Dodoma alipukutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Chama hicho ambao wamechaguliwa tena na Mkutano Mkuu wa Mwezi Mei 2021 Jijini Mbeya kuongoza kwa kipjndi cha miaka mitatu.
“Nawapongeza kwa kuaminiwa na kuchaguliwa, kuingoza TAGCO. Nataka niwasisisitize kuwa mkatekeleze na kusimamia majukumu yenu vyema.
Mshirikiane na Idara ya Habari – MAELEZO, mjadili maazimio ya mkutano wa Maafisa Habari uliomalizika hivi karibuni huko Mbeya na kuweka mikakati na muda wa utekelezaji wake”, ameeleza Mhe. Bashungwa.
Aidha, Waziri Badhungwa ameeleza kuwa utoaji wa taarifa sahihi za utekelezaji wa Serikali ya Awamu ya Sita unahitajika kiliko wakati mwingine wowote hivyo ni muhimu kwa Chama hicho kuongeza kasi ya utendaji ili taarifa za Serikali ziweze kuwafikia wananchi kwa haraka na usahihi.
Fauka ya hayo, Mheshimiwa Waziri amesisiza TAGCO kwa kushirikiana na Idara ya Habari kuandaa mafunzo ya mara kwa mara ya kuwajengea uwezo Masfisa Habari ili waendane na kasi ya mabadiliko katika utoaji wa taarifa kwa njia za kisasa kutokana na kukua kwa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Amewaeleza kuwa Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan inawaunga mkono kwa nguvu zote Maafisa Habari ili waweze kuhakikisha wananchi wanapata taarifa za utekelezaji wa Serikali.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa TAGCO, Bw. Pascal Shelutete amesema kuwa Chama hicho ni kiungo muhimu katika kutoa habari za Serikali kwa jamii kupitia Maafisa Habari pamoja na kuisimamia vyema Kada hiyo muhimu kwa nchi.
“Tunahamu umuhimu wa kada hii na sisi kama Chana kwa kushirikiana na Idara ya Habari tutatekeleza maelekezo yako ili kukidhi matarajio ya Serikali ya Awamu ya Sita”, alieleza Shelutete.
Hivi karibuni Idara ya Wizara ya Habari kwa kushirikiana na TAGCO walifanya Mkutano wa mwaka (Kikao Kazi) ambapo pia ulifanyika uchaguzi wa viongozi wa TAGCO.
Katika uchaguzi huo, Pascal Shelutete alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, Sarah Kibonde (Makamu Mwenyekiti), Abudl Njaidi (Katibu), Gaudensia Simwanza (Katibu Msaidizi), Tabu Shaibu (Mweka Hazina), na Gerald Chami (Mweka Hazina Msaidizi).
Wengine ni Dkt. Cosmas Mwaisobwa (Katibu Mwendzi), Nteghenjwa Hosea (Katibu Mwenezi Msaidizi) na nafasi ya Wajumbe wa Kamati Tendaji ni Innocent Byarugaba, Dickson Msakazi, Karim Meshack na Ally Kondo.