Home Michezo YANGA YAIPAPASA RUVU SHOOTING, YAITUNGUA MABAO 3-2 FEI TOTO ATUPIA MBILI

YANGA YAIPAPASA RUVU SHOOTING, YAITUNGUA MABAO 3-2 FEI TOTO ATUPIA MBILI

0

******************************

Klabu  ya Yanga imefanikiwa  kuinyuka Ruvu Shooting kwa mabao 3-2 kwenye uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam ambapo Feisal Salum ‘Fei toto’ kuibuka shujaa kwa kuweza kupachika mabao  2 kwenye mchezo huo.

Feisal Salum alianza kufungua akaunti ya mabao katika mchezo huo ambapo dakika ya 23 aliweza kufunga bao safi na kumuacha kipa wa Ruvu Shooting ashindwe afanye nini. Bao la pili alipachika dakika ya 32 na kuwafanya kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa mabao hayo.

Kipindi cha pili,  Ruvu Shooting walianza kwa kasi na kupachika dakika ya 70 kupitia kwa Emmanuel Martin kisha Yanga walipata bao la ushindi dakika ya 80 kupitia kwa Saido Ntibanzokiza. 

Ni David Richard wa Ruvu Shooting alipachika bao la kufuta machozi dakika ya 82 na jitihada zao kusaka pointi zilikwama baada ya dakika 90 kukamilika.

Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha jumla ya pointi 64 ikiwa nafasi ya pili huku Ruvu Shooting ikiwa nafasi ya 10 na pointi 37.