Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba akizungumza wakati akifungua mkutano wa 11 wa wadau wa Kahawa Nchini leo Juni 17,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa Nchini, Prof Aurelia Kamuzora akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 11 wa wadau wa kahawa Nchini unaofanyika jijini Dodoma.
Wadau wa zao la kahawa wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa Nchini, Prof Aurelia Kamuzora akizungumza kwenye ufunguzi wa kongamano la wadau wa zao hilo unaoendelea jijini Dodoma.
……………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba amewataka wadau wa Kahawa nchini kutoa mapendekezo ya kuboresha zao hilo ili kuongeza ufanisi kwenye uzalishaji wake.
Kauli hiyo imetolewa wakati akifungua kongamano la 11 la wadau wa kahawa mwaka 2021 lililofanyika leo Juni 17,2021 jijini Dodoma.
Mgumba amesema zao la kahawa ni moja ya mazao ya kimkakati yaliyochaguliwa na serikali hivyo yanatakiwa kubadilika ,kukua ili kuweza kutoa mchango katika jitiahada.
‘’Mazao haya ya kimkakati yanatakiwa kubadilika ,kukua kuweza kutoa mchango katika jitiahada za serikali za kutatua tatizo la ajira ,kuchangia katika ukuaji wa uchumi,ujenzi wa viwanda,kuongeza vifaa vya wakulima na kukuza uchumi wa wakulima ‘’amesema Mgumba
Aidha,Mgumba amesema uzalishaji wa kahawa siyo mzuri kupitia kongamano hilo litasaidia kuondokana na changamoto hiyo kwani limelenga zaidi kujifunza shughuli za maendeleo ya sekta ya kawahawa zinazotekelezwa katika maeneo mengine.
‘’kupitia kongamano hili natumaini mtajadiliana kwa pamoja kutatua changamoto hii ya uzalishaji mdogo hata kule kwangu songwe uzalishaji unashuka siyo kama ilivyokuwa hapo awali’’amesema Mgumba
Amebainisha changamoto zinazoikabili sekta hiyo kuwa ni tija, uzalishaji mdogo, kuyumba kwa bei, ukosefu wa mitaji kwa wakulima na kutokopesheka kwenye taasisi za fedha na hivyo kuwafanya watu kuamini kuwa kilimo hakilipi.
Hata hivyo Mgumba amewataka wadau wa kahama kutumia fursa hiyo kusikiliza kwa makini mawasilisho yatakayotolewa kwenye kongamano hilo na kutoa mapendekezo ya kuboresha zao hilo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa nchini, Prof. Aurelia Kamuzora amesema kuwa kongamano hilo watajadili sababu za baadhi ya wakulima wa kahawa kukimbilia kuuza Uganda ili kushauri serikali kuondoa vikwazo vilivyopo .
‘’Nina historia na zao hili kwani limenisomesha na kunifikisha katika hatua iliyopo’’amesema Kamuzora
Kongamano hilo limekuwakunisha wadau mbalimbali wa kawaha kutoka maeneo tofauti ambapo limekwenda sambamba na kauli mbiu isemayo ‘’uzalishaji wenye tija ndio nguzo ya maendeleo ya sekta ya kahawa’’
Naye kaimu Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Kahawa Primus Kimaryo Kimaryo amesema lengo la kongamano hilo ni kutatua tatizo la tija katika zao la kahawa.