Home Mchanganyiko SERIKALI KUANZISHA UFUGAJI WA KUKU NA SUNGURA MASHULENI

SERIKALI KUANZISHA UFUGAJI WA KUKU NA SUNGURA MASHULENI

0

Mratibu wa Mradi wa USAID Lishe Endelevu Abdon Hamaro akieleza mikakati mbalimbali ya mradi huo ikiwa ni pamoja na kupunguza udumavu hadi kufikia chini ya asilimia tano.

Afisa Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo) Wambura Messo akizungumza na wafugaji wa kuku na sungura waliodhaminiwa na mradi wa USAID lishe endelevu katika kijiji cha mlali wilaya ya kongwa.

Afisa Mifugo kuyoka wizara ya uvuvi na mifugo akiangalia kuku ambaye anafugwa na moja ya wanufaika wa mradi wa USAID lishe endelevu katika kijiji cha mlali wilaya ya kongwa

Mkulima anayenufaika na Mradi wa USAID Lishe endelevu Mayai Dulla akielezea namna elimu aliyopewa ilivyomsaidia katika shughuli zake za kilimo.

Muonekano wa Kuku pamoja na Sungura .

……………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Kongwa

SERIKALI imesema inampango wa kuanzisha ufugaji wa kuku na sungura mashuleni ili kuwajengea wanafunzi elimu ya vitendo na kuongeza ulaji wa mazao yatokanayona mifugo.

Akizungumza mara baada ya kutembelea Mradi wa USAID Lishe Endelevu katika kijiji cha Mlali Wilaya ya Kongwa Afisa Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo) Wambura Messo  amesema  ulaji wa mazao ya mifugo bado uko chini kwa watanzania

“Tayari tumeandaa andiko kwaajili ya kuanzisha  ufugaji wa kuku na sungura mashuleni  lengo tunataka watoto wanaomaliza shule wawe na elimu ya darasani na elimu ya vitendo kupitia ufugaji,

“Tutashirikiana na wadau  mbalimbali ambao watatusaidi kupeleka kuku na sungura  wa kutosha mashuleni  ili wanafunzi waanze kufaidika kwa kula mazao ya yatokanayo na mifugo hiyo kama nyama na mayai,”amesema

Messo alipongeza mradi wa USAID lishe endelevu chini ya Save the Chirdren kwa kuendelea kuwawezesha wananchi kwa kuwapa mifugo kama samaki,kuku,,sungura  mbuzi na mbegu lishe ili kuwainua kiuchumi na kuboresha afya zao kupitia ulaji wa vyakula hiyo.

Kwa upande wake Afisa Lishe Wilaya ya Kongwa Maria Haule amesema mradi wa USAID lishe endelevu utasaidia kupunguza udumavu kwa watoto Kwani wananchi wameanza kubadili mtindo wa maisha.

“Niwashukuru wadau wa USAID lishe endelevu wanaofanya kazi kwenye Halmashauli hii ya Kongwa katika vijiji vyote 87 ambao lengo lao kubwa ni kupunguza kiwango cha udumavu kwa kubadilisha tabia za jamii kuwa na tabia chanya katika masuala ya lishe hasa kwa watoto na wajawazito,

“Tunaamini baada ya mradi huu kuishi huenda kiwango cha udumavu kitakuwa kimepungua kwa kiasi kikubwa baada ya kufanya utafiti

Aliwataka wananchi kutumia vyema miradi hiyo na kubadilika kupitia elimu wanazopewa na miradi hiyo.

Kwa Upande wake Mratibu wa Mradi wa USAID Lishe Endelevu Abdon  Hamaro alisema mradi wa USAID lishe endelevu unatekelezwa Dodoma, Iringa, Rukwa na Morogoro ambao unalenga kutoa elimu ya lishe kwa jamii na kuhamasisha uzalishaji wa chakula mchanganyiko.

Lengo ni kupunguza udumavu, kwa watoto na kwa Jiji la Dodoma Halmashauli ya Kongwa tuna vikundi malezi na kila kikundi tunatoa elimu  na wao wanatoa maoni ambayo wanataka tuboreshe ili huduma hii iende mbali zaidi,

Alisema kwa upande wa kongwa mratibu wa mradi huyo alibainisha kuwa wamefikia vikundi 130

Ambapo kwa mikoa yote waliyoifikia wamepanga kuwafikia  Wanawake milioni moja, vijana 330 na watoto chini ya miaka mitano milioni moja na nusu.

Lengo la mradi ni kuhakikisha kuwa baada ya miaka mitano kuishi udumavu upungue ufikie chini ya asilimia tano na adhima hiyo itatimia kama tutashirikiana na serikali na wananchi wenyewe.