Wa kwanza kulia ni Msemaji wa Jeshi la Polisi SACP David Misime na kushoto kwake ni Mkuu wa Shule ya Polisi Moshi SACP Ramadhan Mungi, wakielekea ukumbini kwaajili ya kufungua mafunzo ya siku tatu kwa maafisa habari wa Polisi yanayofanikia mkoani Kilimanjaro katika shule ya Polisi Moshi. (Picha na Jeshi la Polisi)
Msemaji wa Jeshi la Polisi SACP David Misime katikati kwa waliokaa na kulia kwake ni Mkuu wa Shule ya Polisi Moshi SACP Ramadhan Mungi wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa, wakaguzi pamoja na askari walioshiriki mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa habari wa Polisi nchini yaliyofanyika katika katika Shule ya Polisi Moshi yenye lengo la kuwajengea Mweledi maafisa habari wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi, Mikoa na Vikosi.
(Picha na Jeshi la Polisi)
Msemaji wa Jeshi la Polisi SACP David Misime akipokea taarifa maudhurio ya waandishi wa habari wa Polisi kutoka kwa ASP Richard Minja yaliyofanyika katika Shule ya Polisi Moshi yenye lengo la kuwajengea Mweledi maafisa habari wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi, Mikoa na Vikosi
(Picha na Jeshi la Polisi)
*************************
Msemaji wa Jeshi la Polisi SACP David Misime mapema leo amefungua mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa habari wa Polisi nchini yaliyofanyika katika Shule ya Polisi Moshi yenye lengo la kuwajengea weledi wakutekeleza majukumu yao ya kazi za kila siku ikiwa ni pamoja na kuongeza ushirikiano na wadau wengine. Maafisa habari hao wa Jeshi la Polisi ni kutoka Makao Makuu ya Polisi, Mikoa na Vikosi.
Misime amesema wandishi hao wanafanya kazi katika ofisi za Makamanda wa Polisi mkoa na vikosi wakiwa na majukumu ya kuwasaidia Makamanda kwenye shughuli zote za kihabari ikiwemo kuandaa taarifa kwa vyombo vya habari (Press Releases) ama Press Conferences lakini kutengeneza Dokumentari mbalimbali ambazo zitatumika kutoa elimu kwa jamii.
Aidha Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime aliwataka waliohudhuria mafunzo hayo kushiriki kikamilifu kwa kusikiliza, kuuliza maswali ili kuwa na weledi zaidi katika utendaji wa kazi za kila siku.
Misime alitaja mambo ambayo watafundishwa katika mafunzo hayo ni pamoja namna ya kuundaa na kutoa taarifa kwa waandishi wa habari, mahusiano kati ya waandishi polisi na wadau wengine, namna kuzuia unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto, namna ya kuripoti makosa ya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto,mapambano ya kisaikolojia na habari ambapo kwa ujumla mada zitakazo tolewa ni 14.
Msemaji wa Jeshi la Polisi SACP David Misime alimshukuru mwakilishi wa LSF Fortunata Ntwale (Afisa Program) kwa ushirikiano uliowezesha mafunzo hayo kufanyika.
Naye Afisa Program kutoka LSF Fortunata Ntwale katika ufunguzi huo amesema wamefadhili mafunzo hayo ili kushirikiana na jeshi la polisi ili kuwajengea uwezo wanahabari wao wa kutoa elimu katika kutetea haki za watoto na wanawake kwa kushirikisha wadau wengi zaidi.