Home Mchanganyiko NAIBU WAZIRI MWANAIDI AWATAKA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUIMARISHA MABARAZA YA WATOTO...

NAIBU WAZIRI MWANAIDI AWATAKA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUIMARISHA MABARAZA YA WATOTO NCHINI

0

NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii,Mwanaidi Khamis ,akizungumza wakati akifungua Baraza la Taifa la Watoto lililofanyika leo Juni 14,2021 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii,Mwanaidi Khamis ,akisisitiza jambo wakati akifungua Baraza la Taifa la Watoto lililofanyika leo Juni 14,2021 jijini Dodoma.

Makamu Mwenyekiti wa Bra za la Watoto aliyemaliza muda wake akisoma risala kwa mgeni rasmi Naibu  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii,Mwanaidi Khamis, wakati akifungua Baraza la Taifa la Watoto lililofanyika leo Juni 14,2021 jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi.Vickness Mayao,,akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Taifa la Watoto lililofanyika leo Juni 14,2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Mtoto,Sebastian Kitiku,akizungumza wakati wa  Baraza la Taifa la Watoto lililofanyika leo Juni 14,2021 jijini Dodoma.

Baadhi ya watoto wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii,Mwanaidi Khamis (hayupo pichani) wakati akifungua Baraza la Taifa la Watoto lililofanyika leo Juni 14,2021 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii,Mwanaidi Khamis akiwa katika picha ya pamoja na watoto mara baada ya kufungua  Baraza la Taifa la Watoto lililofanyika leo Juni 14,2021 jijini Dodoma.

……………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii,Mwanaidi Ally Khamis amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii ,kuhakikisha mabaraza ya watoto nchini yanaimarishwa.

Pia amewaomba wazazi na walezi nchini kuwaruhusu watoto kujiunga na mabaraza hayo.

Kauli hiyo ameitoa leo June 14,2021,Jijini Dodoma wakati akifungua Baraza la Taifa la Watoto,ambapo amewataka kuhakikisha Mabaraza ya watoto yanaimarishwa kwa kuhakikisha mambo ya watoto yanazungumzwa pamoja na kutafutiwa suluhu.

”Nitoe wito kwa wazazi na walezi  kuwaruhusu watoto kujiunga katika Mabaraza hayo ili waweze kupata sauti kwenye mambo yao”amesema

Kuhusina na changamoto walizozitoa za bima ya afya na mafunzo  kwa ajili yao,amesema
watazifanyia  kazi kwa mujibu wa sharia za nchi huku akiahidi kuwa  Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa watoto kuhusiana na mambo yao.

Awali Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo anaemaliza muda wake,Aidath Ishulula,akisoma risala kwa niaba ya watoto nchini  amesemakuwa  wanakabiliwa na changamoto za rasilimali fedha katika kuendesha mabaraza,watoto kutokuwa na bima na kutokukamilika kwa mpango kazi.