Home Mchanganyiko KITUO CHA MALEZI,MAKUZI NA MAENDELEO YA AWALI YA MTOTO CHAZINDULIWA CHAMWINO DODOMA

KITUO CHA MALEZI,MAKUZI NA MAENDELEO YA AWALI YA MTOTO CHAZINDULIWA CHAMWINO DODOMA

0

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mwanaidi Ali Khamis,akipata maelezo kutoka kwa Mkufunzi mwezeshaji Mradi wa Yidan Prize(BRAC Maendeleo Tanzania) Bw.Dule Mbua wakati akikagua darasa la watoto wanaolelewa katika kituo cha kijamii cha  malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya watoto kilichozinduliwa leo Juni 14,2021 wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mwanaidi Ali Khamis,akiwasilia katika kijiji cha Chamwino Ikulu Mkoani Dodoma kwa ajili ya kuzindua kituo kijamii cha malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto kwa kushirikiana na Shirika la BRAC Maendeleo -Tanzania leo Juni 14,2021 wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mwanaidi Ali Khamis,akizungumza kabla ya kuzindua kituo kijamii cha malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto kilichojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la BRAC Maendeleo -Tanzania leo Juni 14,2021 wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi.Vickness Mayao,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo kijamii cha malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto kilichojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la BRAC Maendeleo -Tanzania leo Juni 14,2021 wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Mtoto,Sebastian Kitiku,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo kijamii cha malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto kilichojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la BRAC Maendeleo -Tanzania leo Juni 14,2021 wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Mkurugenzi Mkazi Shirika la BRAC Maendeleo- Tanzania Bi.Susan Bipa, akielezea umuhimu wa kushiriki katika ujenzi wa kituo wakati wa uzinduzi wa kituo kijamii cha malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto kilichojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la BRAC Maendeleo -Tanzania leo Juni 14,2021 wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Mtendaji wa Kijiji cha Chamwino Blandina Matagi akisoma taarifa ya ujenzi wakati wa uzinduzi wa kituo kijamii cha malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto kilichojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la BRAC Maendeleo -Tanzania leo Juni 14,2021 wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Baadhi ya waalikwa wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mwanaidi Ali Khamis,(hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa kituo kijamii cha malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto kilichojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la BRAC Maendeleo -Tanzania leo Juni 14,2021 wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Diwani wa Kata ya Chamwino Joseph Seganje,akitoa neno la shukrani wakati wa uzinduzi wa kituo kijamii cha malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto kilichojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la BRAC Maendeleo -Tanzania leo Juni 14,2021 wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mwanaidi Ali Khamis,akiwa na Kaimu Katibu Mkuu Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi.Vickness Mayao wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi wa kituo kijamii cha malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto kilichojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la BRAC Maendeleo -Tanzania leo Juni 14,2021 wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mwanaidi Ali Khamis,akiwa katika [icha ya pamoja mara baada ya kuzindua kituo kijamii cha malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto kilichojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la BRAC Maendeleo -Tanzania leo Juni 14,2021 wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

………………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Chamwino

Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imesema kupitia Halmashauri zote nchini itaendelea kuhamasisha, kuratibu na kusimamia uanzishwaji na uendeshaji wa vituo vya malezi,makuzi na maendeleo  ya awali ya mtoto    kwa kushirikisha wazazi, walezi na jamii kwa ujumla. 

Hayo yamesemwa leo Juni 14,2021 na  Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mwanaidi Khamis wakati akizindua kituo kijamii cha  malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto kwa kushirikiana na  Shirika la BRAC Maendeleo – Tanzania kilichopo katika kijiji cha Chamwino Ikulu Mkoani Dodoma

Naibu Waziri amesema kuwa kwa kushirikiana na wadau wa wa maendeleo Serikali itaendelea kuhamasisha na kuamsha ari ya wananchi ili kushiriki katika ujenzi wa vituo hivyo katika vijiji na mitaa yote nchini ili kuhakikisha kuwa huduma hiyo inapatikana.

”Serikali kupitia halmashauri zote nchini zitaendelea kuhamasisha, kuratibu na kusimamia uanzishwaji na uendeshaji wa vituo  kwa kushirikisha wazazi, walezi na jamii kwa ujumla.”amesema Naibu Mwanaidi

Kuhusiana na kituo hicho,Naibu Waziri amesema kuwa kitasaidia  kuwajenga watoto utimilifu wao ikiwa ni pamoja kuwapatia huduma jumuishi za afya, lishe, ulinzi, ujifunzaji na uchangamshi wa awali kabla ya kujiunga na darasa la awali wanapofikia umri wa miaka 5.

“Huduma hizo zinamwezesha mtoto kukua kimwili, kiakili, kisaikolojia na kimaono akiwa angali mtoto hali hiyo itasadia kuwa na Taifa lenye watu walioandaliwa kikamilifu kulitumikia,”amesema.

Aidha,amelishukuru Shirika la BRACK Maendeleo-Tanzania kwa kushirikiana na Serikali kujenga vituo 30 vya mfano kikiwemo kituo hivyo  ambavyo vipo katika hatua tofauti za ujenzi katika Halmashauri sita.

“Pamoja na faida atakayoipata mtoto moja kwa moja, katika vituo hivyo ni kutoa  fursa kwa wazazi na walezi kupata muda wa kutosha kwa ajili ya kufanya shughuli za maendeleo ya watoto wakiwa vituoni na pia kuwaepusha watoto na hatari mbalimbali,”amesema

Pia, amesema kuwa mtoto asiyepitia katika vituo vya malezi na makuzi ya awali atakuwa tofauti na aliyepitia kwenye vituo kwa kuwa ataimarika katika stadi za kujifunza, ubunifu na uchangamshi kabla ya kujiunga na darasa la awali.

“Watoto wengi hasa wa vijijini ambako hakuna vituo vya malezi wanakosa huduma muhimu za malezi na misingi inayofaa katika maandalizi ya awali ya malezi na makuzi ya mtoto, hivyo kuwafanya baadhi ya wanaomaliza darasa la saba kuwa na uwezo na ubunifu mdogo,”amesema..

“Niwaombe  wadau wote wa maendeleo kushirikiana na serikali katika uanzishaji wa vituo hivyo katika maeneo wanayofanya kazi ili kuhakikisha kila kijiji na mtaa kunakuwa na kituo cha malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kama ilivyoainishwa katika mwelekeo wa serikali ya awamu ya sita katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025,”amesema.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkazi Shirika la BRAC Tanzania Susan Bipa, amesema kuwa shirika hilo lilianza kujikita katika sekta ya elimu kwa watoto wadogo kupitia mradi wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya mototo mnamo mwaka 2016 chini ya ufadhili wa Mfuko wa maendeleo wa LEGO.

Amesema Mradi huo unaojulikana kama BRAC PlayLab, umekuwa ukitekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam na Mbeya ambapo vituo 80 vilitumika kutoa mafunzo kwa watoto zaidi ya 3,600 ambao walihitimu miaka miwili ya mafunzo na asilimia 96 ya watoto hao kuweza kuingia katika shule za awali kwenye maeneo husika.